WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasilisha ujumbe wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano la Uwekezaji wa Sekta ya Misitu linalofanyika katika Viwanja vya Wambi Mafinga, mkoani Iringa.
Akiwasilisha ujumbe huo muhimu, Waziri Mkuu amewaambia wananchi wa mkoa wa Iringa na wote waliohudhuria kongamano "mimi nimekuja na salamu zenu za upendo na baraka tele kuoka kwa kiongozi wetu wa nchi, mpendwa wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan."
Akinukuu maneno ya ujumbe huo Mhe. Majaliwa amesema "Waziri Mkuu, waambie wananchi na wadau wote waliopo kwenye kongamano hilo la uwekezaji kwamba, pamoja na uvunaji tunaofanya ni lazima tukumbuke kupanda miti kwa wingi zaidi, ili kupata faida zote zinazopatikana kutokana na miti tuweze kuzipata." Amesema Majaliwa.
Aidha, amewaambia wananchi kuwa Rais ametoa ujumbe huu kwetu Watanzania lakini pia maalum kwa wanamkoa wa Iringa kupitia kongamano hilo na kusisitiza kuwa ujumbe huo ni wa muhimu sana.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.