• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ukishindwa kusimamia kusoma, kuandika na kuhesabu jitathimini

Imewekwa tarehe: January 5th, 2023

KAIMU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amewataka  viongozi  wanaosimamia elimu  katika Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa kujitathmini katika ufuatiliaji wa mwenendo wa elimu kwa watoto kwa kujua kusoma ,kuandika na kuhesabu wanaomaliza elimu ya msingi.

Dkt. Msonde ameeleza katika Kikao kazi cha Maafisa Elimu wa Mikoa, Wilaya, Taaluma na Watu Wazima kilichofanyika Dodoma.

Amesema kutokana  na tabia ya baadhi ya viongozi kusahau majukumu yao kwa kutowafuatilia walimu sehemu zao za kazi na kushindwa kufanya kazi kwa waledi, inapelekea kutokuwepo kwa ufanisi  katika kazi na matokeo yake kusababisha kutopatikana kwa elimu bora na watoto kumaliza elimu ya msingi kushindwa kusoma, kuhesabu na kuandika.

Aidha, amewataka viongozi hao kutokubali kukabidhiwa watoto kuanzia darasa la awali kutoka kwa wazazi/walezi na  kisha mtoto huyo  amalize darasa la saba kwa kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

“Hilo halitakubalika baadhi ya watu waharibu mipango na malengo ya Serikali, haiwezekani mtoto anamaliza darasa la saba hawezi kusoma, kuhesabu na kuandika ingelikuwa ni mtoto wako kama mzazi utajisikiaje kama kiongozi uliyepewa dhamana ikitokea hivyo maanake jitathmini hutoshi” amesisitiza Dkt. Msonde

Amewataka viongozi hao kutojikweza kwa uongozi na madaraka sababu sio lengo la Serikali bali lengo ni kwenda kushirikiana na walimu kwa kuwafuatilia na kujua changamoto kwa pamoja na kuzipatia ufumbuzi na sio kuwakatisha tamaa walimu.

Dkt. Msonde amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujenga na kuboresha elimu nchini pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia Januari, 2023 watoto wengi wataingia shule fedha zilizotolewa za ujenzi wa madarasa 8000 asilimia 96 yamekamilika tushirikiane na jamii ili  watoto hao waliochaguliwa waingie shuleni.

“Tuna walimu wazuri wakihamasishwa  kwa kupewa motisha, ari na hamasa ya kufanya kazi tutakuwa na taifa bora sababu wataalamu wetu wengi wanatokana  na walimu ” Dkt. Msonde

Kwa upande wake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Paulina Nkwama amewataka viongozi hao kusimamia misingi ya utumishi wa walimu katika kuwafuatilia maadili  na utekelezwaji wa majukumu yao ikiwemo suala la ufuatiliaji wa utoro wa walimu ambao unazorotesha elimu na kama walimu watakuwa vizuri kwa kutekeleza kwa ufanisi, waledi na ubunifu tutakuwa na watu wenye elimu bora nchini.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais- TAMISEMI Vicent Kayombo ametoa rai kwa viongozi hao kwenda kuyasimamia  na kuyatekeleza maelekezo waliyopangiwa na viongozi hao sababu wameaminiwa na ni jukumu lao kusema wanaenda kuleta mabadiliko ya elimu kwa maslahi ya taifa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Msonde amewataka viongozi hao kusimamia kwa kuwaandaa watoto kuanzia darasa la Awali  ili wanapofika darasa la nne na saba wafanye vizuri zaidi na sio kuwaacha mpaka wafike madarasa hayo ndio watumie nguvu kubwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.