HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imeajiri askari wa Mgambo 30 watakaokuwa wanafanya doria katika viunga vya Mji ili kudhibiti watu wanaochafua mazingira kwa kutupa taka ovyo ikiwa ni namna mojawapo ya kuhakikisha mji huo unakuwa safi wakati wote ikizingatiwa ndiyo Makao Makuu ya Nchi.
Hatua hiyo inafuatia kampeni ya usafi wa mazingira iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Daktari Binilith Mahenge ya kufanya usafi siku ya Jumamosi kila wiki.
Akizungumza wakati wa zoezi la usafi mwishoni mwa Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amesema askari Mgambo 30 waliofuzu mafunzo wako tayari na kwamba Manispaa inatarajia kuanza kuwatumia wiki hii ya kwanza ya mwezi Desemba.
Aliwashauri wakazi wa Dodoma na wageni kujiepusha na utupaji wa taka ovyo, na kwamba atakayebainika na kuthibitika kufanya hivyo atatozwa faini kati ya Shilingi 50,000 hadi 300,000 kulingana na mazingira ya tukio papo hapo na endapo atashindwa kulipa atatumikia kifungo cha miezi sita gerezani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.