Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula amewataka watumishi na uongozi wa Hospital ya Mirembe kuhakikisha wanatembea pamoja kwa kudumisha ushirikiano baina yao ili kuleta mabadiliko chanya ikiwemo kuboresha huduma zitolewazo na kuboresha stahiki za watumishi katika hospitali hiyo.
Dkt. Chaula amesema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembeleo hospitali ya Mirembe na kufanya mazungumzo na watumishi ili kujadiliana namna gani watatatua changamoto walizonao katika maeneo yao ya kazi. "Tunatakiwa kukaa pamoja na tutembee pamoja wakati wote, ili kuleta mabadiliko katika Hospaital na taasisi yetu, tuache kulalamika maana sisi sote tulio hapa ndio Serikali yanyewe". Amesema Dkt. Chaula.
Kwa upande mwingine Dkt. Chaula ameagiza uongozi wa Hospitali ya Mirembe kuwa wabunifu kwa kuhakikisha wanasimamia miradi yao vizuri hali itakayosaidia kuongeza makusanyo ya mapato na kulelekea kuboresha huduma za afya na stahiki za Watumishi. "Hospitali inatakiwa iwe ya mfano hivyo mnatakiwa kuongeza jitihada na ubunifu katika utendaji wenu, ikiwemo usimamizi mzuri wa miradi, tunataka kuona mabadiliko ili kuweza kusonga mbele", amesisitiza Dkt. Chaula.
Aidha, Dkt. Chaula ameagiza maboresho katika maabara, huku akiahidi kurudi baada ya wiki moja ili kuona mbaoresho yaliyofanywa, ikia ni seemu ya usimamizi na ufuatiliaji wa maboresho ya huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo. Mbali na hayo, Dkt. Chaula ameto wito kwa watumishi katika hospitali hiyo kwenda katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kujifunza baadhi ya mbinu na ubunifu wanaoutumia katika kuendesha baadhi ya idara zao ili kuleta mabadiliko ya haraka ikiwemo katika suala la ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande mwingine, Dkt. Chulai ameto a wito kwa watumishi katika Hospitali hiyo kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kutenda hadki kwa kutoa huduma kwa usawa kwa wagonjwa wote katika maeno ya kazi.
Picha na matukio:
Chanzo: wizara_afyatz
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.