• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ushuru wa mabango, majengo warudi Halmashauri

Imewekwa tarehe: February 2nd, 2021

SERIKALI imetoa muongozo mpya ambapo kuanzia sasa kodi za majengo, ushuru wa mabango na vitambulisho vya wajasiriamali vitasimamiwa na wakurugenzi wa Halmashauri husika tofauti na awali ambapo vilikuwa vikisimamiwa na Mamlaka ya mapato TanzaniaTRA, ikiwa ni lengo kuimarisha ukusanyaji wa mapato.

Wakitoa kauli ya pamoja kati ya Wizara ya Fedha na Mipango na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa serikali imeamua kutoa madaraka kwa wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia vitengo hivyo kwa kuwa hao ndio wenye wigo mpana zaidi hadi ngazi za Mitaa.

Amesema wakurugenzi wa Halmashauri sasa watakusanya kodi za majengo yote ikiwa na lengo la kuongeza wigo wa kukusanya mapato kutokana na uwanda wa serikali za Mitaa kuwa mpana zaidi na kuyafikia majengo yaliyokusudiwa.

“Tumeamua kukubaliana Wizara hizi mbili kuwa sasa mapato yote yakusanywe na Wakurugenzi wa Halmashauri ili wigo uwe mpana zaidi, kodi za majengo yote zitakusanywa na Wakurugenzi na kuziingiza Serikalini” amesema Waziri Jafo.

Amewataka wakurugenzi kuwashirikisha Maafisa biashara, na watendaji wa ngazi zote kuhakikisha wanasimamia vizuri zoezi hilo liweze kuleta tija kuhakikisha majengo yote yanalipiwa kodi inayositahili na Serikali inapata mapato stahili.

Kuhusu ushuru wa mabango amesema Wakurugenzi watakusanya ushuru wa mabango yote yaliyopo katika maeneo yao yaliyokuwa yakikusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), isipokuwa mabango yanayosimamiwa na Wakala wa Barabara TANROADS na TARURA.

“Mabango yote yaliyokuwa yanasimamiwa na TRA sasa yote yatakuwa chini ya wakurugenzi tunaamini ufanisi utaongezeka kwa kuwa Wakurugenzi wanayajua mabango yote yaliyokatika maeneo yao kila aina ya bango na sehemu lilipo katika eneo hilo tunataka kuona ufanisi mkubwa wa ukusanyaji wa mapato” amesema.

Kuhusu vitambulisho vya wajasiliamali Waziri Jafo amesema vitambulisho vipya vya wajasiliamali tayari vimechapishwa na kupelekwa katika ofisi za TRA kote nchini na sasa vitakuwa chini ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wakavichukue tayari kuwafikia wajasiliamali kote nchini.

Aidha, Mhe.Jafo amesema kuwa vitambulisho hivyo sasa vitasimamiwa na wakurugenzi wa Halmashauri katika kuvifikisha kwa wajasiliamali na kutaka usimamizi madhubuti kuhakikisha zoezi hilo linakwenda vizuri na Serikali inapata mapato.

Amesema vitambulisho hivyo vilivyoboreshwa vitapatikana kwa bei ile ile ya shilingi elfu ishirini (20,000) kwa kitambulisho kimoja kitachomuwezesha kufanya biashara mwaka mzima, na hakuna mjasiliamali yeyote hapa nchini kufanya biashara bila kuwa na kitambulisho.

Hata hivyo Mhe.Jafo amesema kuanzia sasa serikali haitarajii mfanyabiashara kufanya biashara bila kuwa na Cheti cha kulipa kodi ya TRA, leseni ya biashara ya Halmashauri au kitambulisho cha wajasiliamali, hatua kali zitachikuliwa kwa watu kama hao watakaokiuka utaratibu wa kuwa na leseni ama kitambulisho cha mjasiliamali.

Vile vile, ameonya kwa wafanyabiashara wakubwa wanaokwepa kodi kwa kutoa vitu kwenye maduka kwenda kwa wajasiliamali bila kuwa na lisiti ya bidhaa hizo, na kuwa Serikali imeweka mkazo na kuwataka wafanyabiashara kutoa lisiti na mteja anayenunua bidhaa kuhakikisha anadai lisiti.

Amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote kuhakikisha wanasimamia vizuri zoezi hilo kuhakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Serikali yanasimamiwa kikamilifu kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa ya kukusanya mapato ili kuwahudumia wanchi, huku akibainisha maelekezo maalumu ya maagizo hayo watapatiwa katika vikao kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwanaidi Hamis amewasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi stahiki kwa Serikali ili Serikali iweze kujiendesha, na kuwataka wasimamizi katika kodi za majengo, Mabango na Vitambulisho vya wajasiliamali kusimamiwa kikamilifu.

KWA MSAADA WA FULLSHANGWE BLOG

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.