• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Uswiss yaipa Tanzania msaada wa Sh. Bilioni 44.1 kuondoa umasikini

Imewekwa tarehe: October 6th, 2020

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bwana Doto James na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, wamesaini Mikataba  miwili ya msaada wa Faranga za Uswiss milioni 17.8 sawa na Shilingi bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21, jijini Dodoma leo.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Uswisi zimesaini makubaliano ya mikataba miwili ya  msaada ya Faranga za Uswiss milioni 17.8 sawa na Shilingi bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21, jijini Dodoma leo.

Akizungumza mara baada ya kusaini mikataba hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James, amesema kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 39.15 itagharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini chini ya Mfuko Maendeleo ya Jamii (TASAF) 2020 hadi 2023.

Huku mkataba wa pili kuwa ni wa msaada wa Shilingi bilioni 4.95 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa pamoja wa afya kwa mwaka wa fedha 2020 hadi 2021.

”Lengo la program hii ni kuboresha upatikanaji wa fulsa za kujipatia kipato  na huduma za kijamii kwa kaya maskini, kulinda na kuboresha nguvu kazi ya familia zisizojiweza.

”Na lengo la Mpango wa Mfuko wa Pamoja ni kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za afya ya msingi ikiwa ni malengo kuboresha huduma za afya kwa jamii” amesema James.

Akizungumzia mradi wa TASAF amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano tangu mwaka 1960 ambayo inathibitishwa na miradi inayoendelea na iliyokamilika kwa kufadhiliwa na Serikali ya Uswisi.

Amesema msaada huo utasaidia kupunguza umaskini na kuboresha nguvu kazi, kuboresha upatikanaji wa fulsa ya kujipatia kipato kwa kaya maskini na pia kujenga na kulinda nguvu kazi ya watoto wao, na kuongeza uwezo wa kumiliki mali na huduma za kijamii.

Kuhusu mpango wa TASAF Awamu ya Kwanza uliotekelezwa kutoka mwaka 2013 hadi 2019, na ulitelelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 159 Tanzania Bara na Visiwani na kufanikiwa kuzifikia kaya milioni 1.1 zenye watu milioni 5,296,470 kwa kutoa ajira za muda kwa kaya zenye uwezo wa kufanya kazi.

Ameongeza kuwa ”TASAF imeweza kuongeza kipato kwa kaya maskini kupitia kujiwekea akiba na kujihusisha na shughuri za kiuchumi ili kuboresha maisha yao, pia vikundi vya akiba 22,303 vyenye wanavikundi 311,114 viliundwa katika Halmashauri 54 za Bara na Visiwani” amesema.

Akizungumzia programu ya Mfuko wa Pamoja wa Afya utakaowezeshwa kiasi cha Shilingi bilioni 4.95 ameweka wazi kuwa Uswisi ni moja ya nchi zinazochangia sana sekta ya afya hapa nchini na kuwa na mafanikio makubwa hasa kwa watanzania maskini.

Amesema tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya tano kumekuwa na maboresho makubwa katika sekta ya afya na kumekuwa na ongezeko la vituo vya afya ambapo mwaka 2015 vilikuwa 718 hadi kufikia vituo 1205 kwa mwaka 2020.

Kuongezeka kwa Hospitali za Halmashauri kutoka 77 mwaka 2015 hadi hospitali 178 mwaka 2020 ambapo kunaongezeko la hospitali 101 ambazo ziko hatua mbalimbali za ujenzi, kuongezeka kwa zahanati kutoka Zahanati 6,044 hadi kufikia 7,242 kwa mwaka 2020.

Kwa upande wake Balozi wa Uswisi hapa nchini Bw. Didier Chassot amesema ushishirikiano wa nchi hivi mbili ni wa muda mrefu na wataendelea kushirikiana kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

”Utafurahi kujua kuwa watendaji kutoka Uswisi walianza kufanya kazi na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo na baadaye Rais Mwalimu Julius Nyerere katika kuanzisha kati ya vituo vya kwanza vya kutoa huduma ya afya vijijini nchini Tanzania” amesema Balozi Didier.

Aidha amesema kuwa nchi ya Uswisi imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuleta mageuzi ya kisekta yanayolenga kuimarisha utoaji wa huduma muhimu kwa watanzania.

”Takribani theruthi mbili ya misaada ya Uswisi imetolewa kuchangia bajeti ya mifuko ya pamoja ya kisekta na karibia theruthi moja katika mipango ya misaada ya kiufundi pamoja na TAMISEMI, misaada ya kiufundi imechangia kuanzishwa kwa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa na kuendeleza ajenda ya kutokomeza malaria” amesema.

Aidha, amesema kuwa makubaliano ya leo yataruhusu kuendelea kuchangia mpango wa afya kwa wote (Universal Health Coverage) Tanzania katika mwaka huu wa fedha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, wakisaini Mikataba miwili ya msaada wa   Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21, hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, wakibadilishana Mikataba miwili ya msaada wa  Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 mara baada ya kutia saini mikataba hiyo leo jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot (kushoto) wakionesha Mikataba miwili ya msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwenye hafla ambayo imefanyika leo jijini Dodoma.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.