KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana Jumamosi ametembelea na kukagua eneo ambalo Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Uwanja wa Kisasa wa Michezo jijini Dodoma.
Dkt. Abbas amesema eneo hilo lenye ukubwa wa eka zaidi ya 320 ni kubwa mara 10 zaidi ya eneo vilipo viwanja mbalimbali vya Taifa jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa kwa ukubwa huo eneo hilo linaweza pia kutumia kuweka vituo vingine vya shughuli za burudani ikiwemo ujenzi wa ukumbi mkubwa wa michezo ya ndani na sanaa za maonesho (indoor art and sports arena).
Aidha, Dkt. Abbas amesisitiza kuwa ahadi aliyoitoa Rais Dkt. John Magufuli ya kujenga uwanja mkubwa Dodoma itatekelezwa haraka kadiri iwezekanavyo.
Katibu Mkuu Dkt. Abbas alipotembelea eneo ambalo Serikali inakusudia kujenga uwanja mkubwa wa michezo jijini Dodom.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.