NA: WAF, Dar es Salaam
Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametoa rai kwa Wadau wa Maendeleo kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwekeza kwenye Sekta ya Afya nchini huku wakiiga mfano wa Kampuni ya uzalishaji wa Dawa cha Cure Afya ambayo iko mbioni kuanza uzalishaji wa dawa hapa hapa nchini.
Waziri Mhe. Ummy ameyasema hayo leo Disemba 20, 2023 alipo tembelea Kiwanda kipya cha utengenezaji Dawa cha Cure Afya ambacho kipo Wilaya ya Kigamboni Jiijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuona utayari wa Kiwanda hicho kutengeneza Dawa kwa ajili ya soko la ndani ya nchi pamoja na nchi jirani.
“Dawa zinazozalishwa zitarahisisha upatikanaji wake kwa wakati, tofauti na tukiagiza dawa nje ya nchi zinachukua miezi 6 hadi 9 kuweza kufika hivyo inachukua muda mrefu mpaka kufika nchini”. Amesema Waziri Mwalimu.
Amesema serikali imejizatiti kukuza uzalishaji wa dawa wa ndani ili kupunguza gharama ya uagizaji kwani Tanzania ni miongoni mwa nchi nne za Afrika ambazo zinatambulika kwa umahiri kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA na Shirika la Afya Duniani WHO.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Cure Afya Bw. Paresh Ghelani amesema kuwa wako tayari kwa uzalishaji wa dawa kuanzia Januari 2023 ikiwa ni takwa la Serikali katika uwekezaji wa viwanda kwa mahitaji ya nchi ambayo yatakwenda kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa wakati na gharama nafuu.
Haya ni matokeo chanya ya uhamasishaji Fursa za Uwekezaji wa Viwanda nchini yanayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Sekta ya Afya nchini katika kuendelea kuboresha Sekta ya Afya nchini na kuifanya Tanzania kuwa Kituo cha Utalii tiba ukanda wa Afrika Mashariki.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.