Serikali imedhamiria kuendeleza kufanya Vikao vya Mashirikiano ili kufanya tafakari ya pamoja juu ya shughuli zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene katika mkutano wa kwanza wa Vikao vya Mashirikiano katika ngazi ya Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
"Kushirikiana huku hakuepukiki na kwa bahati nzuri serikali zote ni za Chama Cha Mapinduzi lazima tukutane mara kwa mara ili tuweze kutathimini ni namna gani tunatekeza ilani ya Uchaguzi," amesema Simbachawene.
Amesema hiyo ni hatua nzuri tumefikia na ni lazima tuboreshe ratiba zaidi, ili tuende zaidi ya kiwango tunachokwenda sasa.
"Tusiishie kukutana ngazi hii tu, tuweke utaratibu wa uratibu wa kukutanisha makundi na hasa vijana ili waweze kuufahamu Muungano wetu na wauenzi ili uwe na faida iliyokusudiwa na waasisi wetu wa Nchi hizi Mbili," amesema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma amesema Muungano wetu ni wa kipekee na kuendelea kukutana hivi ni kuimarisha mawazo ya waasisi wetu wa Muungano.
"Tunakaa tunazungumza mambo ya Wizara na taasisi zetu lakini tunakumbushana umuhimu wa Muungano na umoja wetu," amesema.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.