VIONGOZI wa Jukwaa la Wanawake Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamewezeshwa mafunzo ya fursa za kiuchumi katika shughuli za biashara, kilimo, upatikanaji wa mitaji, sheria, ujasiriamali, matumizi ya teknolojia na mikopo ya asilimia kumi.
Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa lengo la kuwakutanisha wananawake ili waweze kujadili fursa na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hidaya Mizega, aliwataka wanajukwaa hao kufahamu majukumu yao na sheria katika kuwezesha mafunzo kwa wanawake wengi kwa kufahamu masuala ya uchumi.
Alisema kuwa, viongozi hao wanajukumu katika mitaa na kata zao kuhamasisha shughuli za kiuchumi kwa kuibua miradi mikubwa na mizuri kupitia mikopo ya asilimia kumi ili kukuza ongezeko la uchumi kwa wanawake, kwa kufuata mwongozo mpya ambao umeboreshwa. “Wajumbe wa majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ngazi ya kata ni wale wanavikundi waliopo katika mtaa husika. Kwa mwongozo huu kama mwanamke hayupo kwenye kikundi basi huyo siyo mjumbe wetu. Lakini pia majukwaa haya tumeona kuna changamoto ya nauli na watu kutoka mbali. Hivyo, serikali ikasema hapana kwa maana hiyo vikao hivi vya jukwaa vimetiwa nguvu vifanyike katika ngazi za mitaa. Hivyo, basi, kazi ya kata na halmashauri ni kuratibu” alisema Mizega.
Nae, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Nkuhungu, Ashura Kimwaga, alisema kuwa, majukwaa hayo yanatakiwa kupewa nguvu katika kuwahamasisha wanawake kuibua miradi na kuweza kupata mikopo ya asilimia kumi kwa uharaka zaidi. “Tumekuwa tukiwasumbua sana maafisa maendeleo wa kata na bila kupata taarifa sahihi lakini leo tumepata majibu sahihi na kipi kinapelekea kuchelewa kupata mikopo. Hivyo, tumefurahishwa tulikuwa na kigugumizi lakini tumepewa 'data' kamili. Kwahiyo, tunatakiwa tuvute subira kwa sababu ina malipo” alisema Kimwaga.
Ikumbukwe kuwa, mafunzo hayo yaliwezeshwa kwenye kata 20 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Aliongeza kwa kusema kuwa, kuchelewa kwa mikopo ya asilimia kumi ni kutokana wa mfumo wa benki kutokukamilika na kwa sababu Dodoma Jiji ipo kwenye utaratibu wa kutoa mikopo kwa majaribio kupita mfumo huo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.