Zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura limekamilika leo Jimbo la Dodoma mjini kwa mafanikio makubwa ambapo watu wengi walikuwa wakijitokeza kila siku ili kuboresha taarifa zao na wengine kujiandikisha upya.
Zoezi hili lilianza tarehe 2 hadi tarehe 4 Mei, 2020, lakini kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliokuwa wakijitokeza ili kutekeleza haki hiyo ya kujiandikisha ilibidi Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza kuongeza siku moja zaidi ili kuwezesha watu wote kujiandikisha. Miongoni mwa wananchi waliojitokeza kuboresha taarifa zao ni viongozi mbalimbali wa Serikali ambao wamehamia jiji Dodoma akiwemo Mkurugenzi wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari ambaye alitekeleza haki hiyo katika kituo cha Shule ya Sekondari Kisasa kilichopo katika Kata ya Dodoma Makulu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.