Na OR-TAMISEMI, Dodoma
Serikali imevitaka vyuo vyote nchini kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea ruzuku ya fedha za matumizi yao kutoka Serikali Kuu.
Akihutubia katika mahafali ya 15 tarehe 07 Novemba, 2023 Hombolo nje kidogo ya Jiji la Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Deogratius Ndejembi ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amevitaka vyuo vyote nchini kujiendesha kibiashara kwa kubuni vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na kuwatatumia Watafiti wabobezi kufanya tafiti.
“Chuo hiki kinayo hazina ya Wabobezi wa fani mbalimbali fanyeni utafiti na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kupunguza utegemezi, vilevile endeleeni kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo na shughuli nyingine zinazohusu ustawi wa chuo” alisema Mhe. Ndejembi.
Ndejembi pia alisema azma ya Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alifanya kikao na Watendaji wa Taasisi mbalimbali nchini mwezi Agosti, 2023 ni kuona mashirika ya Umma yanaongeza tija katika uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Mfuko wa Serikali Kuu.
“nasisitiza mashirika na Taasisi za Serikali ziendelee kubuni mikakati ya kuongeza mapato ili faida itumike kuendesha shughuli za Taasisi na kutoa gawio Serikalini, maelekezo haya yanahusu pia jumuiya ya chuo hiki, ongezeni kasi ya kuibua mikakati inayotekelezeka na yenye tija” alisema Ndejembi.
Ndejembi akijibu kuhusu kero ya kuwekwa lami barabara ya Ihumwa hadi Hombolo alisema tayari upembuzi yakinifu umefanyika lakini ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kazi ianze kwa wakati baada ya kukamilika taratibu zote.
Akisoma risala kabla ya hotuba ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) Prof. Joseph Kusilwa alitoa ombi la kupatiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo pacha ya kampasi ndani ya jiji la Dodoma baada ya kupata eneo la ilipokuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuondokana na adha ya kulipa kodi inayofikia shilingi
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.