WAANDISHI wa habari wametakiwa kuwa vipaza sauti kuelezea umuhimu wa Sensa ya watu na makazi kwa wananchi ili wahamasike na kuhesabiwa tarehe 23 Agosti, 2022.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake ya kutembelea mabanda ya maonesho ya shughuli za wakulima na wafugaji katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Dkt. Mkanachi alisema kuwa mwezi Agosti hapa nchini litafanyika tukio la kihistoria, “Tarehe 23 Agosti, itafanyika Sensa ya sita ya watu na makazi. Waandishi wa habari muwe vipaza sauti ili wananchi wahamasike kuhesabiwa” alisema Dkt. Mkanachi.
Kwa upande wake Afisa habari katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Theresia Nkwanga alisema kuwa waandishi wa habari wanawajibu wa kuhamasisha na kuelimisha juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi. “Waandishi wa habari wanawajibu wa kuhamasisha jamii ili ijitokeze kuhesabiwa. Sensa itaisadia serikali kupanga mipango ya maendeleo ambayo italinufaisha taifa kwa ujumla wake kupitia huduma za kijamii zitakazotolewa” alisema Theresia.
Maonesho ya shughuli za kilimo na mifugo mwaka 2022 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Agenda 10/30: kilimo ni biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.