WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameitaka Serikali kuweka kupaumbele zaidi kwenye kutoa Elimu na kufanya Kampeni za huduma ya afya ya akili nchini ili wananchi waweze kutambua tatizo hilo na kupata tiba stahiki.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya afya na masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo kwa niaba ya Wabunge wote walioshiriki kwenye Semina maalum ya utoaji Elimu ya Afya ya Akili, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Bohari kuu ya dawa (MSD) kwa Wabunge iliyofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
“Ni vizuri Wizara ikawa na Kampeni maalum ya kutoa elimu ya afya ya akili ili watu wanapotaka kupata huduma za afya ya akili wajue pa kwenda” alisema Nyongo
Alisema kampeni hiyo inaweza kuratibiwa kupitia vituo vya ushauri wa masuala ya kitaalam kwa njia za simu (Call Centres), vitengo au vituo vya tiba kwa ajili ya kutibu changamoto za afya ya akili.
“Matangazo na Elimu zikitolewa itapunguza unyanyapaa ndani ya jamii, hali ya aibu itapungua kwakuwa watu watakuwa na uelewa na itawafanya watu kujitokeza kwenda kupata huduma hiyo katika vituo mbalimbali” alisema Nyongo.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Mwalimu alisema kuwa, Wizara itaendelea kusimamia huduma za matibabu ya afya ya akili nchini kwa kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma hizo, huku akiwataka wananchi kutoogopa kujitokeza kupata huduma hizo kwa Wataalamu.
“Usione aibu kulia, kulia tiba ya afya ya akili, kwa changamoto ambazo tunapitia ni dhahiri kuwa wananchi wanapata sonona, wanakosa usingizi hizo zote ni changamoto na dalili za afya ya akili” amefafanua Waziri Mwalimu.
Alisema changamoto ya unyanyapaa kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili ni kubwa na hii inaanza kupitia dhana ya mtu akiugua anapelekwa milembe na kuitwa ‘chizi’ ili hali ameenda kupata tiba kama sehemu nyinginezo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.