JUMLA ya wadau 354 kutoka nyanja mbalimbali ya sekta ya Afya wanatarajia kushiriki kongamano la Afya Tanzania Health Summit linalotajia kufanyika Jijini Dodoma Novemba 25-26 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Rais wa kongamano la Afya Tanzania Health Summit, Dkt. Omary Chillo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma.
Aidha Dkt. Chillo ameeleza kongamano hilo ni la Saba kufanyika na lengo ni kujadili uchumi wa kati unavyoendana na nyanja ya Afya nchini.
Dkt Chillo amesema katika kongamano hilo tasisi zisizo za Kiserikali zitatoa mada na kujadili ni jinsi gani hasa wataweza kuboresha afya ya Jamii kwa wananchi.
Kwakuongezea Dkt. Chillo ameeleza kuwa katika mkutano huo watatoa mrejesho wa mikutano mingine iliyowahi kufanyika na kutoa mapendekezo ya Nini hasa kifanyike katika kuboresha sekta ya afya kipindi hiki Cha uchumi wa Kati.
“Msingi mkuu wa kongamano hili ni kubadilisha uzoefu na kuona tunafanyaje kazi hasa kipindi hikitulichoingia uchumi wa Kati katika taifa letu pendwa la Tanzania,” ameeleza Dkt Chillo.
Vile vile Dkt. Chillo amesema kutakuwepo na maonyesho mbalimbali ya masuala ya afya na wabunifu watako shiriki katika kongamano hilo watapatiwa zawadi.
“Natoa wito kwa Watu ambao bado hawajajiandikisha kujiandikisha ili kuweza kushiriki kongamano hilo na kuleta chachu katika sekta ya afya na kuboresha mifumo ya afya zaidi nchini”, amesiaitiza Dkt. Chillo.
Hata hivyo katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof Magula Mchembe na atakayefunga anatarajiwa kuwa katibu Mkuu Mhandisi Joseph Nyamhanga kutoka Ofsi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali na serikali za mitaa (TAMISEMI).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.