• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wadau wa uvuvi wakutana kupitia Mpango Kazi Uvuvi mdogo

Imewekwa tarehe: November 21st, 2020

WADAU wa Sekta ya Uvuvi kutoka maeneo mbalimbali wamekutana kujadili na kupitisha rasimu ya mpango wa kitaifa wa kutekeleza mwongozo wa hiari wa kuhakikisha uvuvi mdogo unakuwa endelevu nchini.

Akiongea wakati akifungua kikao kazi cha kupitia mpango huo wa kitaifa leo Novemba 21, 2020 jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Emmanuel Bulayi alisema sekta ya uvuvi inatoa ajira ya moja kwa moja kwa wavuvi wadogo wapatao 202,053 na zaidi ya wananchi milioni 4.5 wanategemea shughuli zinazohusiana na uvuvi ikiwemo uchakataji na biashara ya samaki na mazao mengine.

Aliongeza kuwa pamoja na hali hiyo bado wananchi wengi wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi ni masikini huku akisema kuwa hali hiyo haikubaliki na ni kinyume na maelekezo ya sera na miongozo mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ya nchi yetu ikiwemo Sera ya Uvuvi ya mwaka 2015.

Bulayi aliendelea kueleza kuwa Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kutatua changamoto zinazowakabili wavuvi ikiwemo uandaaji wa mpango wa kitaifa wa kutekeleza mwongozo wa hiari wa kuhakikisha uvuvi mdogo unakuwa endelevu.

Alisema mwongozo huo umeibua na kutoa njia ambazo zikitumika kikamilifu hali ya kiuchumi na kijamii ya wavuvi wadogo itaboreka kwa kiasi kikubwa huku rasilimali za uvuvi zikiendelea kuvunwa kwa njia endelevu.

“Usimamizi thabiti wa mwongozo huu unaweza kupelekea kuongezeka kwa ajira, kipato, chakula na lishe na hivyo wavuvi wengi kujikwamua katika umasikini uliopitiliza,” alisema Bulayi.

“Nichukue fursa hii kulishukuru sana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mwongozo wa Hiari na kuhakikisha uvuvi mdogo unakuwa endelevu katika muktadha wa chakula na kuondoa umasikini,” aliongeza Bulayi

Aidha, alisema pamoja na mwongozo huo kuwa umepangiliwa vizuri, kama utekelezaji wake hautasimamiwa ipasavyo, hautaweza kutoa tija inayotarajiwa na kwa kutambua hilo Wizara iliunda Kikosi Kazi cha Kitaifa mwaka 2018 ili kusimamia utekelezaji wa mwongozo huo.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dkt. Oliver Mkumbo alisema umuhimu wa mpango kazi kwa nchi ya Tanzania uko wazi ukizingatia sekta ya uvuvi inayotegemewa na watu wengi kwa shughuli mbalimbali za kujipatia kipato na lishe.

“Tunatambua juhudu za Serikali, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zinazotekeleza mpango huu, tunaipongeza serikali na wadau kwa kuona umuhimu wa mpango huu na ni matumaini yangu utasaidia kuleta maendeleo kwa wavuvi na jamii kwa ujumla,” alisema Mkumbo

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kusimamia mazingira nchini (EMEDO), Elitrudith Lukanga aliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa mpango huo na alitoa wito kwa mashirika mengine kuhakikisha wanashiriki vyema katika mchakato wa utekelezaji wa mpango huo.

“Sisi kama sehemu ya wadau wa utekelezaji wa mpango huu tutashiriki kikamilifu katika kuhamasisha wadau mbalimbali hususani Wanawake kuuelewa mpango huu ili uwe sehemu katika shughuli zao za kila siku,” alisema Lukanga

Sehemu ya Wadau wa uvuvi walioshiriki warsha ya kupitisha rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu nchini iliyofanyika Novemba 21, 2020 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Kitaifa, Mpango wa Kitaifa wa Kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu, Alhaj, Yahya Mgawe akieleza jambo katika warsha ya kupitisha rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu nchini iliyofanyika Novemba 21, 2020 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Uvuvi, Stephen Lukanga akiongea na wadau walioshiriki warsha ya kupitisha rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu nchini iliyofanyika Novemba 21, 2020 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Emmanuel Bulayi akiongea na wadau wa uvuvi (hawapo pichani) wakati akifungua warsha ya kupitisha rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu nchini iliyofanyika Novemba 21, 2020 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Emmanuel Bulayi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki warsha ya kupitisha rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu nchini iliyofanyika Novemba 21, 2020 jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka TAMISEMI, Dismas Teti, wapili kutoka kulia ni Mkurugenzi, Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Nazael Madala na watatu kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Uvuvi, Stephen Lukanga. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uvuvi, Merisia Sebastian, wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Kitaifa, Mpango wa Kitaifa wa Kutekeleza Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu, Alhaj, Yahya Mgawe na watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dkt. Oliver Mkumbo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.