MKUTANO wa wafanyabiashara na wawekezaji kati ya Tanzania na Misri umefanyika katika hoteli ya Hyatt Regency leo tarehe 05 Desemba, 2021 kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Misri.
Wafanyabiashara na wawekezaji pia wamepata fursa ya kukutana na Taasisi za Serikali zenye miradi ya kipaumbele ambazo zinafanya kazi moja kwa moja na wawekezaji.
Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe, Waziri wa Biashara (Zanzibar), Mhe. Omar Said Shaaban, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Steven Byabato na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji nchini Misri (GAFI), Mhe. Mohamed Abdel Wahab pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za Serikali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.