• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waganga wakuu wakumbushwa kujitathimini uandikishaji iCHF

Imewekwa tarehe: January 4th, 2021

WAGANGA Wakuu wa Halmashauri zote nchini wamekumbushwa kujitathimini kuhusu uandikishaji wa wananchi kwenye Bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF).

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Ntuli Kapologwe alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na timu za afya za Halmashauri katika Mikoa ya Singida, Tabora na Katavi wakati wa ziara ya kuhamasisha usimamizi shirikishi katika vituo vya kutolea Huduma za Afya.

“Suala la wananchi kujiunga na CHF bado liko chini sana yaani hamfanyi vizuri kabisa katika eneo hili, pasipokuwepo na uwajibikaji wa pamoja na kujitoa kwa dhati ni vigumu sana kufanikiwa katika hili, wananchi wengi wanakosa huduma bora za Afya kwa sababu tu hawajajiunga na Bima hii” amesema Dkt. Ntuli.

Ameendelea kusema kuwa timu za uendeshaji zinapaswa kuweka mikakati ya kufikisha Elimu kwa wananchi na kuwahamasisha kujiunga ili kupunguza gharama za papo kwa papo mara mtu anapougua.

Gharama za kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii ni nafuu sana na zimewekwa zikimlenga mwananchi wa kipato cha chini kabisa ili aweze kupata matibabu mara anapougua aliongeza Dkt. Ntuli.

Nataka kila Mganga Mkuu wa Halmashauri ajitathmini pamoja na Timu yake ya Uendeshaji wa Huduma za Afya je wameandikisha wananchi kwa kiwango gani katika eneo lake kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii alihoji Dkt. Ntuli.

Mikoa inayofanya vizuri kidogo ni pamoja na Dodoma na Morogoro lakini mingi ni ile ambayo uandikishaji uko chini na hauridhishi.

“Miaka ya nyuma Mkoa wa Singida ulikua unafanya vizuri, mpaka maeneo mengine walikua wanaenda kujifunza lakini kwa sasa wameshuka na wako kwenye asilimia tano tu, ni wakati wa kujitathmini kwanini mmeshuka katika uandikishaji na mchukua hatua za makusudi kuhakikisha mnarudi kwenye kiwango chenu cha awali” alisema Dkt. Ntuli.

Aliongeza kuwa kwa ujumla uandikishaji mpaka Kitaifa tumefikia jumla ya kaya 438,882 (sawa na 4.0%) zenye watu 1,871,850 ambapo kwa mwaka huu wa 2021 tunataka tufikie asilimia 20 ya uandikishaji hivyo kila mmoja wetu akasimamie hili liweze kufikiwa.

“Tuwaelimishe wananchi kuwa kuwa wanapijiunha wanafaidikia na mtandao mkubwa wa huduma za tiba katika vituo vyote vinavyomilikiwa na serikali na vya Mashirika ya Dini vyenye Makubaliano ya kutoa huduma, kuanzia zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Hospitali za Rufaa za Mikoa.

Mwanachama anapojiunga na Bima ya Afya ya Jamii atapata huduma katika vituo takribani 6,000 nchi nzima ikiwemo Zahanati 4,922, Vituo vya Afya 716, Hospitali za Wilaya 179 na Hospitali za Mikoa 28 na anatibiwa popote nchini bila kizuizi.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

    May 25, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.