• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wagonjwa 6 mfumo wa umeme kwenye moyo watibiwa JKCI

Imewekwa tarehe: May 4th, 2021

WAGONJWA sita wenye matatizo ya hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo ambao mapigo yao ya moyo yanakwenda haraka kuliko kawaida (Tachyarrhythmia’s) wamepata matibabu katika kambi maalum ya matibabu hayo iliyomalizika hivi karibuni  katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Kambi hiyo ya siku mbili ilifanywa na madaktari wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mtaalamu mbobezi wa moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo Dkt. Yona Gandye alisema katika hali ya kawaida moyo hupiga kati ya mapigo 60 hadi 100 kwa dakika.

Dkt. Gandye alisema mtu akiwa na tatizo katika mfumo wa umeme wa moyo ambalo anaweza kulipata aidha kwa kuzaliwa nalo au athali ya ugonjwa linapelekea mfumo wa umeme wa moyo kubadili mapigo yake inaweza kuwa chini ya mapigo 60 kwa dakika au kuwa juu ya 100 kwa dakika.

“Sababu mbalimbali zinaweza kuufanya moyo udunde kwa haraka kuliko kawaida hii ni pamoja na mtu kuzaliwa na tatizo, kwa kurithi kutoka  kwa wazazi hata kama wao hawakuwa na dalili. Sababu ya pili ni ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, moyo kutanuka na  kuwa na misuli mikubwa ya moyo (Hypertrophy).

“Mgonjwa anakuja kliniki akiwa na dalili za moyo kushindwa kufanya kazi ambazo ni miguu kuvimba, pumzi kubana, kushindwa kulala vizuri usiku. Ukimfanyia vipimo unakuta moyo wake umetanuka na umefika mahali umeme wake wa moyo haufanyi kazi vizuri”, alisema Dkt. Gandye.

Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo Prof. Mervat Aboulmaaty kutoka Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri alisema amefurahi kuona taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imefunga mtambo wa kisasa wa Cathlab ambao umeungaishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System wenye uwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Prof. Mervat alisema, “Kufungwa kwa mashine hii ya kisasa na yenye teknlologia ya hali ya juu kutaweza kuokoa maisha ya watu wengi wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo nchini Tanzania”,.

Alisema katika katika kambi hiyo licha ya kutibu, wataalamu walibadilishana ujuzi wa jinsi ya kutibu wagonjwa wenye tatizo hilo la moyo unaokwenda kwa haraka.

Aliongeza kuwa kupitia Chuo Kikuu cha Ain Shams cha nchini Misri wanatoa elimu kwa njia ya mtandao kuhusu matibabu hayo ambapo madaktari wengi wa Afrika wakiwemo wa Tanzania wamekuwa wakishiriki.

“Hii ina maana kuwa baada ya miaka michache ijayo tutakuwa na madaktari wengi wenye utaalamu wa kutoa matibabu ya hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo ambao mapigo yake yanakwenda haraka kuliko kawaida na kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa wenye matatizo haya”, alisema Prof. Shams ambaye pia ni mkufunzi katika chuo hicho.

Naye mtaalamu mbobezi wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Reuben Mutagaiwa ambaye alishiriki katika kambi hiyo alisema waliandaa wagonjwa ambao walikuwa na dalili za ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo baada ya kuwachunguza kwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Stress Electrocardiography – ECG) waligundulika kuwa na tatizo.

“Ili kuchunguza na kubaini zaidi kuna vipimo ambavyo vinafanyika kwa kitaalamu vinajulikana kama Electrophysiological (EP) studies & ablation ambapo mgonjwa anaingizwa katika chumba cha upasuaji (Cathlab) kwa ajili ya uchunguzi wa mfumo wa umeme wa moyo (electrophysiology) unasisimua yale matatizo ambayo yalionekana katika kipimo cha ECG (Induction of Arrhythmias) baada ya kuuleta umeme wa moyo ambao hauna upangilio unaweza kufahamu ni upande gani umeme huo unatoka na kuweza kuudhibiti”, alisema Dkt.Mutagaiwa.

Dkt. Mutagaiwa alisema baada ya kugundua kama  tatizo liko kwenye upande wa kushoto au wa kulia wa moyo kuna kifaa maalum kiitwacho Ablator ambacho kinatoa joto na ukiliweka sehemu ambayo umeme wa moyo hauna mpangilio unatoka unaweza kumtibu mgonjwa kwa kuziunguza njia hizo.

“Kwa kawaida wagonjwa hawa walikuwa wanawekwa katika dawa za vidonge lakini dawa zinaukomo wake, hadi wanafanyiwa matibabu haya walishashindikana kwenye dawa hivyo basi matumizi ya dawa tuliyasimamisha na kuwafanyia tiba hii”.

“Faida kubwa ya tiba hii ni mgonjwa kupona moja kwa moja na baadaye mgonjwa anashauriwa kutumia dawa na kuendelea na kliniki yake kama kawaida”, alisisitiza Dkt. Mutagaiwa.

Matibabu hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza katika maabara ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo (Catheterization Laboratory – Cathlab) mpya ambapo mwanzoni mwa mwaka jana Serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya kufunga mtambo huo ambao umeunganishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System wenye uwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Matibabu ya tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo ambao mapigo yake yanakwenda haraka kuliko kawaida (Tachyarrhythmia’s) yalianza kutolewa hapa nchini mwaka 2019 ambapo hadi sasa wagonjwa 11 wameshapata matibabu.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.