• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wakandarasi Wasiomaliza Miradi Mashakani

Imewekwa tarehe: February 9th, 2025

Na. Faraja Mbise, DODOMA

TARURA imeagizwa kuwasimamisha wakandarasi wasiokamilisha miradi kwa wakati na wasipewe tena miradi hiyo kwasababu wanakwamisha juhudi za Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati na ya kimaendeleo nchini.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa (Mb) alipokuwa akizungumza na wataalam kutoka taasisi mbalimbali za kiserikali pamoja na wananchi wa Jiji la Dodoma katika Hafla ya utiaji saini mkataba wa uboreshaji Soko Kuu la Majengo pamoja na ujenzi wa Kituo cha Daladala eneo la Mshikamano, Kizota na Nzuguni, uliofanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

“Maelekezo yangu kwa TARURA, mkandarasi huyu asiruhusiwe kufanya kazi yoyote chini ya TARURA kuanzia sasa mpaka akamilishe mradi huu tunaoukusudia. Nendeni makafanye tathmini, mniletee taarifa maramoja” alielekeza Mchengerwa.

Kauli hiyo, ilifuatiwa mara baada ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (Mb) kutoa lalamiko la kutokukamilika kwa mradi uliokabidhiwa tarehe 23 Septemba, 2023, Mkandarasi huyo alipatiwa kiasi cha fedha Milioni 24 kwa awamu ya kwanza na kutakiwa kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Sambamba na hilo alitoa agizo kwa wakandarasi wote nchini, ambao hawakamilishi miradi yao kwa wakati uliowekwa katika mikataba wasiruhusiwe kupewa kazi yoyote. “Mkandarasi huyu na wengine ambao hawajakamilisha miradi hii ambayo ilipaswa ikamilike mwezi Februari wasiruhusiwe kupewa kazi yoyote hata ya shilingi 500. Hatuwezi kuwa na watu ambao hawawezi kuona fikra za Rais wetu anatafuta fedha, analeta fedha, na bado wanakuwa goigoi hatuwezi kukubali hata kidogo. Maelekezo yangu kwa Mkandarasi huyu na wengine wa aina hii wasiruhusuiwe kufanya a kazi kokote ndani ya TARURA” aliagiza Mchengerwa.

Aidha, alitoa maelekezo mahususi kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuweka utaratibu mzuri wa watu wa kuingia na kutoka katika Stesheni ya reli ya mwendokasi (SGR), Samia Suluhu Hassan, Dodoma,  kwa sababu Jiji la Dodoma ndio makao makuu ya nchi.

“Ninawataka wakurugenzi wote wa majiji lakini hasa Jiji la Dodoma ambalo ndio makao makuu ya nchi, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya nendeni mkajipange hasa pale eneo la Stesheni ya reli, utaratibu wa watu kuingia na kutoka haujakaa vizuri, makakae pamoja na TRC muweke utaratibu mzuri. Haieleweki na Rais wetu hawezi kutuelewa, yeye ameleta fedha, ninyi wajibu wenu ni kuwasaidia watanzania ili waweze kupata njia nzuri ya kuingia kwenye Stesheni ya reli. Sasa ninawataka ninyi na TARURA mkajipange vizuri, mkazungumzeni na wizara ya uchukuzi ili kuweka utaratibu watanzania wanaokwenda na kurudi kutoka Dodoma waweze kuingia na kupita vizuri eneo lile” alisema Mchengerwa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata Ya Makole, Omar Omar, alimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mikakati mizuri ya kuboresha miundombinu ya Jiji la Dodoma na kukemea wakandarasi wote ambao hawatekelezi miradi yao kwa wakati. Aidha, alitoa wito kwa wakandarasi kusimamia na kutekeleza miradi kwa wakati.

“Tumeona namna alivyokuwa anazungumza, kuonesha ukali namna ambavyo atataka kustawisha makao makuu ya nchi Dodoma, hususani katika suala la maendeleo  na upangiliaji wa mji wa Dodoma nampongeza pia kwakuwa amekuwa mkali kwa wakandarasi wavivu ambao wanapewa kazi na kutoweza kutekeleza kwa wakati. Rai yangu ninawasisitiza wakandarasi wote ambao wamepewa agizo hili waweze kufanya kazi zao kwa wakati na miradi kutekelezeka kwa wakati” alitoa rai Omar.

Nae mfanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo, Samiri Majid , aliunga mkono agizo la waziri Mchengerwa la kuwasimamisha wakandarasi wasiotekeleza miradi yao kwa wakati na akatoa rai yake kwa wakandarasi wote na kusisitiza watangulize uzalendo mbele badala ya maslahi yao binafsi.

“kwa upande wangu nianaona jambo hilo ni jema kwasababu wakandarasi wa namna hiyo wanachelewesha sana maendeleo ya taifa letu. Rai yangu kwa wakandarasi ni kwamba wakati wakikabidhiwa ‘share’ ya mradi wajitahidi kufanya kazi hiyo kama walivyokuwa wanahitaji kupewa kufanya hiyo kazi, kwasababu mkandarasi atakapokuwa anahitaji kupata ‘share’ atatumia mbinu yoyote ile kuhakikisha anapata. Hivyo niwaombe watangulize uzalendo mbele, maslahi ya nchi mbele na wasitangulize maslahi yao binafsi ili taifa letu lizidi kukua na kuwa taifa linalojengeka kadri siku zinavyokwenda” alisema Majid.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.