• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wakurugenzi watakiwa kujitathmini ukusanyaji wa mapato

Imewekwa tarehe: January 25th, 2021

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ameiagiza Mikoa ambayo Halmashauri zake zimekusanya mapato chini ya asilimia 50 kufanya tathmini na kuweka mikakati madhubuti katika ukusanyaji wa mapato katika vipindi vilivyosalia.

Waziri Jafo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/21 kwa kujumuisha taarifa ya mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani vya Halmashauri kuanzia Julai hadi Desemba, 2020.
Waziri huyo alisema wakurugenzi wa Halmshauri zote ambazo hazijafikia asilimia 50 ya makisio kwa kipindi hiki cha nusu mwaka wanatakiwa kujitathmini na kuweka mikakati mizuri ya kufikia malengo katika ukusanyaji wa mapato.

Aidha, alisisitiza kila Halmashauri kuendelea kutumia kwa usahihi mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na mifumo ya uhasibu ili kutoa taarifa kwa kufuata matakwa ya kisheria na kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta za Umma (IPSAS).

Akizungumzia ukusanyaji wa mapato hayo Waziri Jafo alieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/21 Halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 814.96 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Desemba, 2020. Kwa kipindi hicho Halmashauri zimeweza kukusanya jumla ya shilingi bilioni 381.27 sawa na asilimia 47.

Alifafanua kuwa taarifa za mapato ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri katika kipindi cha Julai - Desemba, 2020 imeonesha uwepo wa ongezeko la mapato yaliyokusanywa kuwa ni shilingi bilioni 24.5 ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa katika kipindi kama hicho cha Julai - Desemba, 2019 sawa na ongezeko la asilimia 7.

Waziri Jafo ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 88 ya makisio yake ya mwaka wakati Halmashauri za Wilaya za Kishapu na Longido zikiwa za mwisho kwa kukusanya chini ya asilimia 20 ya makisio yake ya mwaka.

Katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi bilioni 30.67 na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imekusanya mapato kidogo kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Milioni 324.89.

Hata hivyo katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia asilimia ya makusanyo Waziri Jafo alibainisha kuwa Mkoa wa Katavi umefanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo umekusanya kwa wastani wa asilimia 62 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo wakati Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Simiyu ambao umekusanya wastani wa asilimia 36 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameweka wazi ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri kimkoa kwa kuzingatia wingi wa mapato kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri kwa kigezo cha wingi wa mapato ambapo umekusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 89.13 huku Mkoa wa mwisho katika wingi wa mapato ni Mkoa wa Rukwa ambao umekusanya Shilingi Bilioni 4.07.

Vile vile Ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri kwa kuzingatia aina ya Halmashauri kwa kigezo cha asilimia ya makusanyo ukilinganisha na makisio ya mwaka Waziri Jafo alisema kwa upande wa Majiji Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 50 ya makisio yake ya mwaka na Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya kwa asilimia 39 ya makisio yake ya mwaka.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeongoza kundi la Halmashauri za Manispaa ambayo imekusanya asilimia 69 ya makisio yake na katika kundi hilo Halmashauri ya Manispaa ya Singida imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya kwa asilimia 29 ya makisio yake ya mwaka.  

“Kwa kundi la Halmashauri za Miji, Halmashauri ya Mji wa Kahama imeongoza kwa kukusanya kwa asilimia 67 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo Halmashauri ya Mji wa Bariadi imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 23 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2020/21” alisema Waziri Jafo

Aidha, kwa upande wa Halmashauri za Wilaya amesema Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeongoza kwa kukusanya asilimia 88 ya makisio ya mapato ya ndani huku Halmashauri za Wilaya za Kishapu na Longido zimekuwa za mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya chini ya asilimia 20 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa Fedha 2020/21.

“Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa kundi la Halmashauri za Majiji kwa kigezo cha wingi wa mapato kwa kukusanya Shilingi bilioni 18.53 na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi bilioni 5.66.” alieleza Waziri Jafo

Kwa kuongezea Waziri Jafo alisema kwa upande wa Halmashauri za Manispaa, Manispaa ya Ilala imeongoza kwa kukusanya Shilingi bilioni 30.70 na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 834.53,

Huku katika kundi la Halmashauri ya Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 4.78. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 324.89

Chanzo: Tovuti ya TAMISEMI

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

    May 25, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.