• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Walimu Jijini Dodoma washauriwa kuchanja chanjo ya Korona

Imewekwa tarehe: October 5th, 2021

WALIMU wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni watu muhimu katika kutoa elimu na uhamasishaji kwa jamii ili iweze kufanya maamuzi sahihi katika kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 unaosababishwa na virusi vya Korona.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweli alipokuwa akiongea na maelfu ya walimu wa Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Shekimweli alisema kuwa uongozi wa wilaya umeamua kukutana na kutoa elimu kwa kundi la walimu kutokana na umuhimu wao katika jamii. “Sote tunafahamu kuwa dunia imepata tatizo la ugonjwa wa UVIKO-19 unaosababishwa na virusi vya Korona. Walimu hawajapewa msamaha kupata ugonjwa huu. Tulifikiri kama viongozi wa wilaya tupate muda wa kutafakari pamoja. Tunafahamu kuwa kuna kundi la walimu waliopata ugonjwa huu. Tahadhari zinachukuliwa ila bado kuna maambukizi na vifo” alisema Shekimweri.

Alisema kuwa mwalimu akipoteza maisha ni hasara kwa familia yake na taifa kwa ujumla. “Ndugu zangu, ukiangalia kundi linalokutegemea na dhamana yako kwa jamii na darasa lako unalolipenda una wajibu wa kufanya maamuzi sahihi. Kila mmoja atafakari na kuchukua hatua kwa hekima. UVIKO-19 ni jambo la kufa na kupona, tusichukulie kwa mzaha” alisisitiza Shekimweli.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa walimu ni kundi muhimu sana katika kuelimisha jamii ili ifanye maamuzi sahihi. “Walimu mkielewa vizuri suala la chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19, mnaweza kuelimisha bodi na kamati za shule” alisema Shekimweri.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alisema kuwa ugonjwa wa UVIKO-19 upo katika Jiji la Dodoma na njia za kukabiliana nao ni kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kuachiana nafasi. “Ndugu zangu pamoja na njia hizo, tunayo chanjo ya ugonjwa huo. Tumeshuhudia ndugu zetu wakiugua ugonjwa huu na kufariki. Tumeshuhudia vifo vya watumishi na marafiki zetu. Kuna vifo vya watumishi wa Afya vilivyotokana na wao kuwahudumia wagonjwa wa UVIKO-19. Tumeshuhudia vifo vingi vya walimu wetu kutokana na kutekeleza majukumu yao” alisema Dkt. Method kwa uchungu.

Baadhi ya walimu wa Jiji la Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweli (hayupo pichani) katika uwanja wa Jamhuri.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method (aliyesimama) akiongea na walimu wa Jiji la Dodoma (hawapo pichani) kuhusu njia za kujikinga na Korona, kushoto ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rweyemamu. 

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.