• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Walimu wakuu Dodoma Jiji wapata Mafunzo ya NeST

Imewekwa tarehe: January 21st, 2025

Na. Faraja Mbise, DODOMA.

WALIMU wakuu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamepatiwa mafunzo juu ya ununuzi kwa njia ya mtandao serikalini yatakayoboresha utendaji kazi na kuwawezesha kupata mafundi na watoa huduma kupitia mfumo wa ununuzi ‘NeST’ (National e-Procurement System of Tanzania).

Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 21 Januari, 2025 kwa walimu wakuu wa shule za msingi na yanafanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga chini ya usimamizi wa  Kitengo cha Ununuzi na Ugavi cha Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Vincent Odero alisema kuwa mfumo wa manunuzi serikalini kwa njia ya kielektroniki ni mfumo mzuri na umerahisisha mchakato mzima wa manunuzi na umeleta ufanisi mkubwa katika ununuzi wa umma katika maeneo mbalimbali. “Mfumo huu ni mzuri, umerahisisha mchakato wa ununuzi ambapo taratibu zote za ununuzi hufanyika ndani ya mfumo. Mfumo huu umeleta ufanisi katika ununuzi wa umma kupitia maeneo mbalimbali” alisema Odero.

Kuhusu umuhimu wa mfumo wa ununuzi serikalini, alieleza namna ambavyo mfumo umerahisisha utendaji kazi tofauti na mfumo uliokuwa unatumika awali. “Mfumo wa ununuzi umeongeza uwazi na usawa katika mchakato wa ununuzi, kila mzabuni ana haki sawa ya kuwasilisha zabuni na umepunguza muda wa mchakato wa zabuni. Hivyo, kusaidia ununuzi kufanyika kwa muda mfupi, umepunguza mianya ya rushwa, umeboresha utunzaji wa taarifa za michakato ya ununuzi, umeongeza uwajibikaji kwa watumishi wa umma kwasababu mfumo unaonesha kila hatua ya ununuzi na kupunguza gharama za michakato ya zabuni kwa taasisi na wazabuni” alisisitiza Odero.

Sanjari na hayo alielezea kuhusu agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waraka wa Hazina Namba 2 wa Mwaka 2023/2024, alisema kuwa, unaelekeza watumishi wote wa umma wanahusika na mchakato wa ununuzi ndani ya taasisi za serikali kupatiwa mafunzo yatakayowawezesha watumishi kutumia mfumo wa NeST kwa ufasaha. “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 27 Julai, 2023 ilitoa Waraka wa Hazina Namba. 2 wa Mwaka 2023/24 kuhusu matumizi ya mfumo wa usimamizi wa ununuzi wa umma kwa njia ya kielekroniki ‘NeST’, ambao ulielekeza kwamba, watumishi wote wa umma wanahusika na mchakato wa ununuzi ndani ya taasisi za serikali wapewe mafunzo yatakayowawezesha kutumia mfumo kwa ufasaha. Halmashauri ilitekeleza jukumu hilo kwa kuwawezesha maafisa ununuzi na ugavi kupata mafunzo hayo” alisema Odero.

Aidha, aliwataka walimu wakuu kutokiuka sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA). “Kaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na za Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) zinazofanyika kila mwaka, zimebaini kuwepo kwa mapungufu katika taratibu za ununuzi unaofanyika ikiwemo ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo inayotolewa. Mapungufu haya yamekuwa ni sababu kubwa ya upotevu wa fedha za serikali na miradi mingi kushindwa kukamilika na iliyokamilika kutokuwa na ubora unaotakiwa. Hivyo, niwaombe kufuata kanuni na taratibu zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) alisisitiza Odero.

Mkuu huyo wa kitengo alisema kuwa katika mafunzo hayo washiriki watafundishwa kuandaa mpango wa ununuzi wa mwaka, kuanzisha manunuzi na kuandaa nyaraka za zabuni kwenye mfumo. Maeneo mengine ya mafunzo aliyataja kuwa ni kufanya ufunguzi wa zabuni, kufanya tathmini, kutunuku zabuni na kuandaa mkataba kwenye mfumo, aliongeza.

Vilevile, alisema kuwa, watumishi hao wameaminiwa na kukabidhiwa na serikali jukumu la kufanya na kusimamia ununuzi wa umma katika vituo vyao vya kutolea huduma. Pia alisema kwa atakaekiuka sheria na kanuni hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo faini ya shilingi 10,000,000, kwenda jela miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeandaa mafunzo kwa mara nyingine kwa watumishi wote kutokana na maelekezo ya serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa halmashauri zote nchini kutumia ‘NeST App’ kwa manunuzi yote yanayofanyika ofisi kuu na katika vituo vya kutolea huduma.

Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Vincent Odero

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.