WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa maelekezo kwa wanafunzi 337 ambao matokeo ya mitihani yao ya kidato cha nne mwaka 2022 yamefutwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu kuomba kurudia tena Mitihani hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 11,2023 Jijini Dodoma Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda, amesema kati ya wanafunzi 337 ,wanafunzi 333 walifutiwa matokeo kutokana na udanganyifu huku wanafunzi 4 wakifutiwa matokeo kutokana na kuandika matusi katika mitihani yao.
"Tungesema hawa wanafunzi warudie mitihani na wenzao wa kidato cha nne kwa utaratibu wa kawaida kama ilivyozoeleka serikali ingepata hasara zaidi ya Bilioni moja ila kwa utaratibu huu wa kuomba wenyewe kama na kufanya mtihani huo pamoja na wenzao wanaofanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu kwa utaratibu utakaowekwa na NECTA basi itasaidia sana kupunguza gharama,"
Prof.Mkenda amebainisha kuwa utaratibu wa kurudia mitihani hiyo kwa wanafunzi hao utakwenda sambamba na mitihani ya kidato cha sita ambao unatarajiwa kuanza Mei 2,2023, hivyo watawekewa utaratibu wa kuchanganyika pamoja wakati wa kurudia mitihani hiyo.
Pia amewataka watanzania kwa kukemea kwa pamoja matukio ya wizi wa mitihani kwani inafundisha watoto udanganyifu na wizi, inaondoa uweledi na kuwanyima haki watahiniwa ambao hawajashiriki katika wizi huo ila wamefaulu kwa jitihada zao wenyewe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.