• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waliotumia vibaya Fedha za Lishe wachukuliwe hatua- Rais Samia

Imewekwa tarehe: September 30th, 2022

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwachukulia hatua wale wote waliotumia vibaya fedha za lishe na kukwamisha malengo ya serikali katika kukabiliana na changamoto za lishe nchini.

Agizo hilo alilitoa alipokuwa akihutubia halfa ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji wa shughuli za lishe tukio lililofanyika katika ukumbi wa kisasa wa mikutano wa jengo la kitega uchumi la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililopo Mji wa serikali Mtumba jijini hapa.

Rais Samia alisema “nakuagiza Waziri wa TAMISEMI, wote waliotumia vibaya fedha za lishe au kuzitumia kwa malengo tofauti wachukuliwe hatua na ripoti yake niipate”.

Akiongelea lengo la halfa hiyo, alisema kuwa ni kutatua matatizo ya lishe nchini. “Ndugu zangu, lengo ni kutatua matatizo ya lishe yaliyopo katika maeneo yenu na hasa wanajamii, kuelimisha na kuhamasisha umma kuhusu masuala ya lishe na lishe bora kwa kutumia jumbe mbalimbali na kutoa ushauri kwa wananchi na hasa makundi yanayolengwa” alisema Rais Samia. 

Kuhusu umuhimu wa lishe bora, alisema kuwa ni muhimu kwa jamii hasa wajawazito, watoto na wanawake walio katika umri wa uzazi, wazee, na vijana katika rika ya balehe. “Sasa ukitizama tunaanza na wajawazito kuwapa lishe bora ili watoe watoto wenye afya. Lakini mtoto mwenye afya akisha kuzaliwa tunahitaji kumtunza mtoto huyo nae akifika umri, akiitwa balehe anahitaji kutunzwa pia. Anahitaji kutunzwa ili kama ni mwanamke au mwanaume waje wazae pia watoto wenye afya. Sasa tuangalie ulimwengu wetu sasa hivi. Mama mjamzito tunahangaika nae, watoto wakishazaliwa hawawezi kujisaidia, inaeleweka lazima tuwatunze, watoto balehe. Hebu tufanye utafiti tunakosea wapi? Kwa nini wanakuwa na lishe mbovu?

Kwa nini kunakuwa na changamoto ya lishe, je ni mitindo ya maisha nataka niwe ‘sixpacks’, nataka sijui niwe ‘slim’, nisizidi kilo ngapi…wakifika wakati wa kuwajibika kuja kuzaa kuongeza ‘society’ wanahangaika. Mara supu ya pweza…Tunatatizo na mnalijua mnalificha. Watafiti fanyeni utafiti. Tunatatizo na tatizo hili kwa sababu halisemwi ni siri linaumiza zaidi vijana wetu, mara ndo udongo wa kongo…tatizo kubwa liko kwenye lishe” alisisitiza Rais Samia.

Akiongelea ukubwa wa tatizo la lishe, Rais Samia alisema kuwa matokeo yake ni kuwa na taifa goigoi. “Nasema haya kwa sababu nilishasema kwamba tukiacha hali hii tunaenda kuwa na taifa goigoi. Tunaenda kuwa na taifa lenye watu na si rasilimali watu, ni watu ambao ni mzigo kwa taifa siyo watu ambao watazalisha kwa ajili ya taifa. Kuzalisha mali, kusimamia uchumi, lakini pia kuzalisha watu ili taifa hili liendelee, tutafika pahali hapa hatumjui mke nani mume nani” alisema Rais Samia kwa masikitiko.

Akimkaribisha Rais Samia kuhutubia, waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa alianza kwa kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ujenzi wa ukumbi bora na wa kisasa kwa hadhi ya makao makuu. “Ukumbi huu ni bora na unapendeza na tupo hapa ‘very confortable’. Tuwapongeze sana wenzetu upande wa Jiji la Dodoma” alisema Bashungwa.

Akiongelea shughuli ya tathmini ya 6 ya utekelezaji wa mkataba wa lishe alisema kuwa mkataba huo ni utekelezaji wa agizo la Rais. “Utekelezaji huu uliuasisi mwenyewe mwaka 2017/2018 na ulielekeza usimamizi na utekelezaji wa shughuli za mkataba wa lishe ufanywe na waheshimiwa wakuu wa mikoa” alisema Bashungwa.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.