• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wanafunzi 148,127 kujiunga Kidato cha Tano, Vyuo vya Ufundi

Imewekwa tarehe: June 2nd, 2021

JUMLA ya Wanafunzi 148,127 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2021, ambapo wasichana 63,878 na wavulana 84,249 ya wanafunzi waliofanya mtihani Kidato cha nne mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dodoma pamoja  maafisa elimu mkoa kwa njia ya mtandao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu alisema kuwa hiyo ni baada ya kufanya uchambuzi na kuona kuwa wamekidhi vigezo.

Aidha, Waziri huyo ameainisha tahasusi za masomo kwa wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano ambapo wanafunzi   41,504 watajiunga kusoma tahasusi za Hisabati na Sayansi na wanafunzi 46,159 watasoma tahasusi za masomo ya sanaa na biashara.

“Muhula wa kwanza wa masomo utaanza Mwezi Julai 5,2021 na atakayechelewa kuripoti watapangiwa wanafunzi wengine” alisema.

Matokeo ya Kidato cha Nne 2020 yanaonesha kuwa watahiniwa wa shule waliopata Daraja la I – III walikuwa 153,464 wakiwemo wasichana 67,135 na wavulana 86,329 sawa na asilimia 35.06 ya watahiniwa waliofanya mtihani.

“Watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) waliofaulu kwa Daraja la I - III ni 479 wakiwemo wasichana 289 na wavulana 190” alisema.

Idadi hiyo ya wanafunzi wenye sifa imejumuisha wanafunzi wenye Mahitaji Maalum 288 wakiwemo Wasichana 123 na Wavulana 165.

Aidha, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ni 287 wakiwemo wasichana 149 na wavulana 138.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwaka 2021, ni kutoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na waliosoma nje ya nchi ambao matokeo yao yamefanyiwa ulinganifu wa Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA).

Jumla ya wanafunzi 87,663 wakiwemo wasichana 41,885 na wavulana 45,778 sawa na asilimia 59.18 ya wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule 476 za Serikali zikiwemo shule mpya 42, kati yao wanafunzi wenye mahitaji maalumu walikuwa 288 wakiwemo wasichana 123 na wavulana 165 sawa na asilimia 100% ya wenye Mahitaji Maalum waliokuwa na sifa za kujiunga na Kidato cha Tano.
Wanafunzi 1,598 wakiwemo wasichana 592 na wavulana 1,006 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo vinne vya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Jumla ya wanafunzi 55,308 wakiwemo wasichana 21,401 na wavulana 33,907 wamechaguliwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali za ngazi ya Astashahada na Stashahada (Certificate and Ordinary Diploma) katika Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo Wanafunzi 2,235 wakiwemo
wasichana 1,162 na wavulana 1,073 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya
ngazi ya Stashahada.

 Alisema kuwa wanafunzi 5,757 wakiwemo wasichana 2,798 na wavulana 2,959 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu ngazi ya Astashahada ya Elimu Maalum, Awali, Michezo, Msingi na Ualimu wa Shule zinazofundisha kwa kutumia Lugha ya Kiingereza (English Medium).

 “Wanafunzi 1,709 wakiwemo wasichana 737 na wavulana 972 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu ngazi ya Stashahada ya Sayansi, Hesabu na TEHAMA. Vilevile, Wanafunzi 45,607 wakiwemo wasichana 16,704 na wavulana 28,903 wamechaguliwa kujiunga na
Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika Kada mbalimbali.

Waziri Ummy alisema Serikali ya Awamu ya Sita ingependa kuona wanafunzi wote waliochaguliwa kwenda Kidato cha Tano wanajiunga kwa pamoja ndani ya muda uliopangwa.

“Serikali inawahimiza Wanafunzi ambao wameshakata shauri kujiunga na shule za binafsi kuthibhibitisha kujiunga na shule hizo kupitia mfumo wa “Selform” uliotumika wakati wa kubadilisha tahasusi” alisema.

Aidha, alisema wakuu wa shule za Binafsi ambazo wanafunzi watadhibitisha kujiunga nazo, watatakiwa kuthibitisha kuwatambua wanafunzi hao kupitia mfumo wa “Selform”. Nafasi zitakazopatikana kwa njia hii zitajazwa na wanafunzi kwenye “Second Selection” ili nao waweze kujiunga na shule kwa muda sawa na wenzao.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerard Mweli alisema zaidi ya shule mpya 10 zimeongezeka hali  iliyowezesha wasichana wote kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

 

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.