• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wanafunzi 1,674 watangazwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili

Imewekwa tarehe: August 29th, 2019

Jumla ya wanafunzi 1,674 kati ya wanafunzi 1,861 waliokuwa wanasubiri chaguo la pili la kujiunga na kidato cha tano, wamepewa nafasi hiyo baada ya kuwa na sifa zinazotakiwa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi wa wanafunzi katika chaguo la pili ( Second Selection).

Amesema kuwa wanafunzi 187 wameshindwa kuchanguliwa kutokana na tahasusi (combination) zao kutokuwa na ulinganifu unaotakiwa.

Mhe. Jafo amesema kuwa kati ya wanafunzi 1,674 waliochaguliwa ni wanafunzi 1,497 ambao wamepangiwa masomo ya sanaa na biashara wakati wanafunzi 178 watajiunga na masomo ya sayansi na hisabati.

Akifafanua zaidi amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika shule walizochaguliwa kuanzia Septemba 2 hadi 16 mwaka huu na kuwa watakaoshindwa kufanya hivyo watakuwa amepoteza nafasi hiyo.

“Pia nitoe wito kwa wanafunzi 187 ambao wameshindwa kuchaguliwa kwasababu ya tahasusi zao kutokuwiana (balance) waombe kusoma kwenye vyuo vya ufundi ambayo vinasimamiwa na Baraza la Vyuo vya Ufundi (NACTE).

Hivi karibuni Jafo alitangaza uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano awamu ya kwanza na kubainisha kuwa jumla ya wanafunzi 108,644 ambao ni sawa na asilimia 98.31, walichaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi ikiwa ni kati ya wanafunzi 110,505 wenye sifa.

Mhe. Jafo alisema kuwa kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 69,356 ambapo wasichana ni 31,809 na wavulana 37,547 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano ambao ni sawa na asilimia 62.76 ya wanafunzi 110,505 ya waliokuwa na sifa.

Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano ni 35,703 waliochaguliwa tahasusi ya Sayansi na Hisabati, kati yao wasichana ni 14,876 na wavulana 20,827 huku wa tahasusi ya Sanaa na Biashara ni 33,653, wasichana wakiwa ni 16,934 na wavulana ni 16,719.

Waliojiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi (vipaji maalum) ni 1,462 ambapo wasichana ni 646 na wavulana 816. “miongoni mwao wanafunzi 6 ni wenye mahitaji maalumu ambao wasichana ni watatu na wavulana watatu.

Alisema wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliochanguliwa ni 157 ikiwa wasichana ni 74 na wavulana ni 86, wakati wanafunzi waliochanguliwa ambao waliosoma chini ya taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ni 174 ikiwa ni wasichana 74 na wavulana 100.

Aidha Mhe. Jafo ametoa wito kwa wanafunzi waliopangwa awamu ya pili kuripoti kuanzia tarehe 2 Septemba, 2019 na wanafunzi watakaoshindwa hadi kufikia tarehe 16 Septemba, 2019 atakuwa amepoteza nafasi yake


Chanzo: Tovuti ya OR-TAMISEMI (Kidato cha Tano awamu ya pili

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.