• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wanafunzi watakiwa kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia

Imewekwa tarehe: February 13th, 2024

Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO

WANAFUNZI wa shule za msingi mkoani Dodoma wametakiwa kutoa taarifa kwa Dawati la Jinsia na Watoto pindi watakapofanyiwa ukatili wa kijinsia ili kuwa na jamii isiyo na ukatili wa kijinsia.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Theresia Mdendemi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Dodoma alipokuwa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamwino katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mdendemi alisema “watoto wazuri msisite kutoa taarifa kwa Dawati la Jinsia na Watoto katika Jeshi la Polisi na watu mnaowaamini pindi mnapofanyiwa ukatili wa kijinsia. Hakikisha ndani ya saa 72 mmetoa taarifa kwenye Dawati la Jinsia na Watoto au mtu mnaemwamini ili tuweze kupata Ushahidi. Mtuhumiwa tunatakiwa tumuunganishe kosa alilofanya na ushahidi tutakaopata toka kwenye mwili wako”.

Alisema kuwa mara nyingi ukatili umekuwa ukifanyika kwa watu wa karibu jambo linalofanya mara nyingi matukio hayo kutoripotiwa. “Kwa hiyo tunatoa rai, awe baba au mama, awe shangazi au mjomba, awe mama wakufikia au baba wakufikia, amefanya ukatili toa taarifa mapema ili tuweze kulishughulikia” alisisitiza.

Alisema kuwa kutoa taarifa mapema kutawawezesha kuwaepusha watoto waliofanyiwa ukatili na magonjwa yanayoambuliza.

“Unapotoa taarifa mapema unatoa mwanya kwa sisi kuweza kukusaidia wewe usipate magonjwa yanayoambukiza mfano maambukizi ya virusi vyua ukimwi, mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa. Naimani kwa ujumbe huu mtakuwa mpo tayari kushirikiana na dawati la jinsia kwa kutoa taarifa sahihi, hata kama haumfahamu jina aliyekufanyia ukatili ila ukamtaja kwa muonekano kwa mfano alionekana ni mweupe, ana masharubu, anaongea rafuzi flani, huo ndio utoaji taarifa sahihi. Lakini mnapokuwa barabarani mmekuwa mkifanyiwa ukatili, angalia rangi ya gari, muonekano wa gari pia shika namba za gari” alisema Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mdendemi.

Kwa upande wake, Cpl. Edith Siwango kutoka Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma aliwataka wazazi kutenga muda kuzungumza na watoto wao. “Tupo hapa kwa ajili ya kuwalinda watoto wetu. Wazazi mlio hapa nawaomba mtenge muda wa kuzungumza na watoto wenu ili wawe wanaelewa. Kuwachapa watoto siyo suluhisho, kuongea nao na kuwaelimisha ndiyo suluhu. Kumuelekeza mtoto ndiyo suluhu kwa maisha ya sasa. Kama unataka mtoto wako awe msikivu ongea nae, tusiwaachie walimu peke yao, tukiongea nao watatueleza changamoto zao” alisema Cpl. Siwango.



Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.