WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima amewaomba wanamichezo kupitia Vilabu vyao kuungana na Serikali kupaza sauti ya kuhamasisha wananchi kudhibiti mmomonyoko wa maadili unaochochea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwa watoto.
Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito huo alipokutana na rais wa Klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Said jijini Dar es salaam ikiwa na mwanzo wa ziara yake ya kutembelea vilabu vya Michezo kuhamasisha kada hiyo kushiriki kampeni ya ZIFIUKUKI (Zijue Fursa, Imarisha Uchumi, Kataa Ukatili, Kazi lendelee)
Akiilezea kampeni hiyo Dkt. Gwajima amesema lengo ni kuelimisha jamii kuhusu fursa mbalimbali za uwezeshaji kiuchumi eneo ambalo wananchi wengi wanaonekana kutofahamu husuan ni wa viijijini kwakuwa mifumo ya taarifa haiwafikii.
Waziri Dkt. Gwajima amesema Ajenda ya kulinda maadili ya jamii ni Jambo mtambuka ndani ya taifa, hivyo ni muhimu sekta zote ikiwemo ya vilabu vya Mipira, na Sanaa mbalimbali kupitia majukwaa yao pamoja na mitandao ya kijamii kulikemea kwa nguvu zote.
Ameongeza kwamba, Wizara inaimarisha ushirikiano na jamii ili ajenda hizo zimilikiwe na jamii yenyewe.
Tamasha la hilo ni muendelezo wa Kampeni ya Wizara ya Twende Pamoja Ukatili Tanzania sasa Basi iliyozinduliwa mwaka 2018 kwa sura ya Matamasha ya kuelimisha Jamii kuhusu fursa za Kiuchumi sambamba na kuhamasisha jamii kudhibiti mmomonyoko wa maadili na kupinga ukatili wa kijinsia.
Tamasha hilo litakalo ifikia mikoa yotelitazinduliwa 27 Aprili 2023 Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa kuona umuhimu wa kushirikisha Klabu za Michezo na kwamba, ajenda hiyo ni muhimu na Klabu ya Soka ya Yanga ipo tayari kutoa ushirikiano wote kuhakikisha maadili ya jamii ya kitanzania yanaimarika na wananchi wote wanatambua fursa za kiuchumi na kunufaika ili kuunga mkono juhudi za Serikali.
Katika hatua nyingine, uongozi wa hajismanara TV ambayo ina ushirikiano wa karibu na Klabu ya Soka ya Yanga imeunga mkono ajenda hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.