• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wananchi chukueni tahadhari - Waziri Ummy Mwalimu

Imewekwa tarehe: October 5th, 2022

WAZIRI wa Afya ,Ummy Mwalimu amewatoa hofu Watanzania kuhusu Ugonjwa wa Ebola uliopo nchi jirani na kuwataka waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya kukagua utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Mkoa wa Kagera wakati akipokea taarifa ya Mkoa huo kukabiliana na mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila.

"Tunatakiwa kuongeza jitihada za kuzuia ugonjwa huo usiingie hapa nchini,niwakumbushe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote tunazoelekezwa na wataalamu wa afya kama vile kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni,kutokugusana mikono na uonapo dalili nenda kituo cha kutolea huduma za afya".

Hata hivyo Mwalimu alisema Wizara ya Afya itaendelea kutoa elimu kwa umma kwa Watendaji wote wa Vijiji, Kata na Tarafa pamoja na kutoa mafunzo kwa Waganga wa Tiba Asili ili kutambua mtu mwenye dalili za magonjwa ya mlipuko.

Aidha, Mwalimu amesema Waganga Wafawidhi 351 wa Vituo vya kutolea huduma za afya katika Mkoa wa Kageran watapewa mafunzo ya kukabiliana na Mlipuko dhidi ya Ugonjwa wa Ebola.

“Tutaupa kipaumbele Mkoa wa Kagera katika kukabiliana na tishio hili kwani mkoa huu eneo kubwa linapakana na nchi nyingi” amesema Waziri Ummy na kuahidi kufanya mazoezi ya utayari ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko (Simulation Exercises).

Kwa upande mwingine Mwalimu amewaahidi kuwapatia magari matati (3) ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ili kuokoa maisha kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka mkoa hapo.

Naye, Mkuu wa Mkoa huo Albert Chalamila amemuomba Waziri Ummy kujengewa kituo maalumu cha kutenga wahisiwa wa magonjwa ya mlipuko (Isolation Center)katika mpaka wa Mulongo pamoja na Wilaya ya Ngara-mpaka wa Rusumo, Murusagamba na Kabanga.

Hata hivyo Chalamila ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuipatia hospitali ya Rufaa ya Mkoa CT-Scan pamoja na vifaa tiba vingine ambapo vimeanza kusimikwa hospitalini hapo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.