Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE
WANANCHI wa Kata ya Chang’ombe wanajivunia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi katika kata yao jambo litakaloondoa uhalifu na kuwahakikishia usalama wao na mali zao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy alipokuwa akiongea na wanachama wa CCM na wananchi wa Kata ya Chang’ombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvi jijini Dodoma.
Iddy alisema kuwa Diwani wa Kata ya Chang’ombe, amekuwa akiipambania kata hiyo katika miradi mbalimbali ya maendeleo. “Ndugu wanachama wa CCM na wananchi, Diwani wenu Bakari Fundikila amekwenda kusimamia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe. Kituo kile takwimu zinaonesha baada ya Makao Makuu ya Polisi Wilayaya Dodoma, kinachofuata ni kituo hiki cha Polisi Chang’ombe. Na tumemsikia Diwani hapa amesema kituo hiki mmekijenga wanachama wa CCM na wananchi wa Chang’ombe kwa nguvu zenu wenyewe. Mheshimiwa Diwani tunazidi kukupongeza kwa kazi nzuri” alisema Iddy.
Kijana Issa Mwenda mkazi wa Changombe alisema kuwa ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe utaongeza hali ya usalama kwa wakazi na mali zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.