Na. Mussa Richard, TAMBUKARELI
Diwani wa Kata ya Tambukareli jijini Dodoma, Juma Michael, amesema kuwa ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejenga barabara ya kiwango cha lami inayoanzia ‘Shoppers’ hadi Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma kwa lengo la kupunguza msongamano na kurahisisha huduma ya usafiri.
Diwani Michael, alisema hayo baada ya kutembelewa na waandishi wa habari ofisini kwake kwa lengo la kujionea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye Kata ya Tambukareli kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Kipindi cha nyuma tulikuwa na changamoto ya barabara, lakini tunaishukuru sana serikali imeweza kusikia kilio chetu na kuweza kutujengea barabara yenye kiwango cha lami. Barabara ambayo imekuja kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla, kwasababu hapo awali wafanyabiashara walikuwa wana shindwa jinsi ya kufikisha bidhaa katika maeneo yetu kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara. Lakini kwasasa, wanachi wa Kata ya Tambukareli wanapata mahitaji yao yote kwa uharaka na kwa wakati kutokana na ubora wa miundomninu” alisema Michael.
Nae, Daudi Jackson, mwananchi Kata ya Tambukareli, akaishukuru Serikali kwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo. “Ujenzi wa barabara hii umekuwa na manufaa makubwa kwa sisi wananchi wa Kata ya Tambukareli, kwa sababu kwasasa tunaweza kusafirisha bidhaa zetu kutoka mjini kuja Tambukareli kwa haraka. Pia, tunaweza kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, pia barabara hii inasaidia kufika kwa haraka kwa magari ya dharura pindi linapotokea janga kama moto au kuna mgonjwa anaehitajika kufika hospitali kwa haraka” alisema Michael.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.