• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wananchi waaswa kutumia fursa zinazotolewa na benki za ndani ya nchi

Imewekwa tarehe: January 27th, 2023

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), amewataka Wananchi hasa wa Makundi maalum kutumia fursa zinazotolewa na benki za ndani ya nchi ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza wakati alipotembelea benki ya NMB Makao Makuu Jijini Dar es salaam, Dkt. Gwajima amebaini fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo na ambazo zimewanufaisha makundi maalumu wakiwemo Wanawake, Wamachinga na Waendesha Bodaboda wanaofikia idadi ya maelfu.

Dkt.Gwajima amesema, amefarijika kuona benki hiyo inafanya jitihada ya kurahisisha huduma za kibenki kwa Makundi Maalumu hasa yanayosimamiwa na Wizara hiyo.

"Nimekuja kujifunza ni kitu gani nitawaambia hawa Makundi Maalum hasa ikizingatiwa kwamba, tuko kwenye utekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kama ilivyoelekezwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara tu alipoingia madarakani" amesema Dkt. Gwajima.

Ameongeza pia, moja ya mambo muhimu katika programu hiyo ni jinsi gani utekelezaji wa uwezeshaji wanawake kiuchumi unavyoendelea kwenye sekta mbalimbali ikiwemo mabenki ambapo NMB ni mojawapo ya benki zenye hisa kubwa Serikalini.

Aidha, Dkt. Gwajima ameipongeza NMB kwa kupiga hatua na kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Aidha, ameahidi kuendelea na ziara yake kwenye benki zote sambamba na kuelimisha na kuhamasisha jamii itambue fursa hizi na kuchukua hatua za kujiendeleza kiuchumi jambo ambalo pia litachangia kwenye kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto utokanao na migogoro ya kiuchumi.

Dkt. Gwajima anaendelea na ziara hiyo katika benki nyingine nchini kwa lengo la kuangalia fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi hususani Makundi maalum na kuhakikisha kwa nafasi yake anazisemea ambapo ameitambulisha ziara hiyo kama Operesheni *"Zijue Fursa, Imarisha Uchumi Kataa Ukatili, Kaziiendelee".*

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Ruth Zaipuna amesema benki hiyo ina fursa nyingi kwa Makundi yote katika Jamii ambazo zikitumiwa kikamilifu, zitawainua wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.