• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wananchi washauriwa kusikiliza elimu na hamasa ya Dodoma Jiji Mtaa kwa Mtaa Uchaguzi Festival

Imewekwa tarehe: November 25th, 2024


Na. Asteria Frank, DODOMA

Wananchi wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kusikiliza elimu inayotolewa na wahamasishaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa njia mbalimbali ikiwemo kikundi maalum cha ngoma cha Dodoma Jiji Mtaa kwa Mtaa Uchaguzi Festival.

Hayo, yalisemwa na Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Desdery Kuzenza alipokuwa akihamasisha wananchi kujitokeza kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura na kuwachagua viongozi watakaowafaa kwa manufaa ya maendeleo ya mitaa yao. “Naomba nitoe rai kwa wakazi wa Dodoma na  maeneo mbalimbali waendelee kushiriki  katika ‘program’ mbalimbali za elimu kwa umma ambazo zinalenga kuwaelimisha kuhusiana na umuhimu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na nafasi za uongozi wa serikali za mitaa katika maisha yao ya kila siku na tunasema kwamba serikali za mitaa kwa sauti ya wananchi. Hivyo, wajitokeze kupiga kura kwa maendeleo ya mitaa yao na karibuni kushiriki katika tamasha hili la Dodoma Jiji Mtaa kwa Mtaa Uchaguzi Festival” alisema Kuzenza.

Aidha, mmoja wa wasanii katika kikundi cha DOTI, Salum Ramadhani alisema jukumu lao kubwa ni kuwaelimisha wananchi kuhusiana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hususani tarehe 27 Novemba, 2024 wajitokeze kwa wingi kwenye kupiga kura kwaajili ya kumchagua kiongozi atakaewaongoza mtaani kwao. “Sisi ni wanakikundi wa DOTI, tumeanzia kuzunguka maeneo mengi sana katika mitaa ya Dodoma mjini kama Swaswa mnarani, Ntyuka, Nkuhungu Boda, Mwatano na sehemu mbalimbali kwa lengo la kuwahimiza wananchi wajitokeze kupiga kura kwa njia ya maigizo na ngoma” alisema Ramadhani.

Akipongeza juhudi zinazofanywa na Dodoma Jiji Mtaa kwa Mtaa Uchaguzi Festival, mkazi wa Kata ya Ntyuka, Maige Paul, alisema amefurahi ujio wa Mtaa kwa Mtaa Uchaguzi Festival na hiyo inaonesha kwamba wananchi wote tunatakiwa kwenda kuchagua viongozi wanaounda serikali za mitaa akiwemo mwenyekiti na wajumbe wake watano. “Mtaa kwa Mtaa inaendelea kutufurahisha lakini pia inaendelea kutuhamasisha kwamba, jukumu linalofata ni kubwa ambalo tunatakiwa kwenda kuchagua viongozi ambao watatuletea maendeleo katika kata zetu pamoja na mitaa yetu” alisema Paul.

Akiongelea kuhusu wananchi kujitokeza kupiga kura, mkazi wa Kata ya Ntyuka, Latifa Hamadi alitoa rai yake kwa wakina mama na vijana ambao wana sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi siku ya kuchagua viongozi na kushauri elimu hii isiishie mtaani kwao tu bali ifike na sehemu nyingine. “Nawaomba wakina mama na vijana waliofikisha miaka 18 waende kupiga kura inapofika tarehe 27 Novemba, 2024. Tumependa ujumbe tuliopata katika hamasa hii, lakini pia nawashauri waende kata nyingine nyingi za Jiji la Dodoma kama Kata ya Kilimami, Mkonze na Hazina” alisema Hamadi.

Tamasha la uhamasishaji la Jiji la Dodoma Mtaa kwa Mtaa Uchaguzi Festival linafanywa kwa njia ya kitamaduni na sanaa mbalimbali kwa kutumia maigizo, uchezeshaji ngoma za asili na wasanii nguli wakitumbuiza katika mitaa nyakati za mchana, jioni na usiku  ili kuwafikia wananchi wote wakiwa mitaani kwao na kwa wale wanaoshinda kazini wakirudi waweze kupata burudani pamoja na ujumbe wa elimu ya umuhimu wa kuchagua viogozi watakaoongoza katika mitaa yao.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.