Watanzania wamekumbushwa kuzingatia kanuni za afya na kuchukua tahadhari ili kuweza kujikinga na magonjwa ya mlipuko kufuatia kuanza kunyesha kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam na kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu.
Tahadhari hiyo imetolewa leo na Prof. Abel Makubi Mganga Mkuu wa Serikali , Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
“Kufuatia mvua hizi, ni wazi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Kipindupindu, kuhara damu, na yale yanayoenezwa na mbu ikiwemo ugonjwa wa Malaria na Dengue, endapo wananchi hawatazingatia kanuni za afya na kuchukua tahadhari mapema” Alisema Prof. Makubi
Prof. Makubi amesema kufuatia kujitokeza kwa uharibifu wa miundo mbinu ikiwemo ile ya kusafirisha na kuhifadhia maji safi na taka hali hiyo ina hatarisha afya ya jamii na hivyo kuongeza uwezekano wa kusababisha kuenea kwa urahisi kwa magonjwa ya kuambukiza na yale ya mlipuko.
Aidha, Mganga Mkuu huyo amewakumbusha wananchi kuzingatia kanuniz za afya kwa kuchemsha maji kabla ya kunywa au kuyatibu kwa dawa maalumu na kuhakikisha maji ya kunywa na yale ya matumizi ya nyumbani yanahifadhiwa katika vyombo safi
“Tunawapongeza wananchi na ninyi wanahabari kwa kuendelea kutoa elimu katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu kwa sababu wananchi wamekuwa wasikivu na kutii masharti ya usafi na jinsi ya kujikinga, ni zaidi ya mwaka na nusu sasa Tanzania tumeweza kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu nchini”.
Vile vile, amesema jitihada kubwa za maboresho ya miundombinu ikiwemo kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa maji safi na salama na ushirikiano mzuri wa wananchi na hivyo kusababisha baadhi ya magonjwa yanayotokana na uchafu kupungua.
Hata hivyo, Prof. Makubi amesisitiza kutumia ipasavyo vyoo na hasa kipindi hiki cha mvua kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni mara kwa mara hasa, kabla ya kula, baada ya kula na baada ya kutoka chooni...
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.