• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wanawake wajasiriamali wahimizwa kurasimisha biashara zao

Imewekwa tarehe: November 19th, 2021

WANAWAKE Wajasiriamali wametakiwa kurasimisha biashara zao ili waweze kutambulika na kupata fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali  pamoja na taasisi zake zikiwemo taasisi za kifedha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa ameyasema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kongamano la Wajasiriamali Wanawake kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, lililofanyika kwa lengo la kuenzi Siku ya Mwanamke Mjasiriamali Duniani.

“Naomba nitumie fursa hii kuwashauri na kuwasisitiza kuwa ni muhimu kurasimisha biashara zenu kwakuwa kuna manufaa makubwa utayapata kutokana na urasimishaji kuliko kufanya biashara katika hali zisizo rasmi," alisisitiza Bw. Nyaisa.

Bw. Nyaisa ameainisha baadhi  ya faida za urasimishaji biashara kuwa ni pamoja na biashara kutambuliwa na Serikali, wateja na jamii kwa ujumla, kuongeza fursa za  kupata huduma za Serikali, kurahisisha upatikanaji wa mitaji kutoka serikalini na taasisi za kifedha kama vile mabenki na taasisi zinazotoa mikopo.

Amezitaja faida nyingine kuwa ni kupata huduma mbalimbali za Serikali kama vile, mafunzo, msaada wa kitaalamu na kiteknolojia.

Ameongeza kuwa endapo biashara itarasimishwa inaiwezesha Serikali kuboresha mipango yake ya kuwahudumia wajasiriamali na wafanyabiashara kwa kuwa inakuwa na uelewa wa idadi kamili ya wajasiriamali au wafanyabiashara waliopo.

"Urasimishaji biashara pia unasaidia kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwa walipa kodi wazuri na washiriki wenza wa Serikali katika kutoa huduma kwa jamii," alifafanua Bw. Nyaisa.

Aliongeza kuwa biashara inaporasimishwa inaongeza uaminifu kwa wateja kutokana na kutambulika na Serikali hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuingia mikataba ya kibiashara ama ubia na wafanyabiashara wengine pamoja na  Makampuni ya ndani na nje ya nchi sambamba na  kurahisisha upatikanaji wa dhamana kutoka Serikalini au taasisi binafsi.

Aidha, Bw. Nyaisa amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wajasiriamali katika ujenzi wa uchumi endelevu, ukuaji wa biashara na kuongeza ajira kwa jamii ya Watanzania.

Kutokana na umuhimu wa wajasiriamali  Bw. Nyaisa ameeleza kuwa  Serikali inaendelea kufanya maboresho mbalimbali ya kisera, kisheria, kanuni, taratibu na mifumo ya utoaji huduma kwa  kuzifanya kuwa wezeshi na rafiki kwa wafanyabiasha wakubwa na wadogo ili waweze kurasimisha biashara zao na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotokana na urasimishaji huo.

"Wanawake wengi wamekuwa wakifanya biashara nyingi ndogondogo na nzuri na wamekuwa wakibuni nembo za biashara zao na kuzitumia kwa muda mrefu  lakini ajabu ni kwamba hawazisajili , hali hii imepelekea baadhi ya watu kunakili majina ya biashara hizo na nembo na kuja BRELA kuchungulia kama zimesajiliwa na iwapo hazijasajiliwa basi wanasajili na kuzitumia , hali hii imesababisha wahusika kufikisha malalamiko BRELA," amefafanua Bw.Nyaisa.

Bw. Nyaisa aliongeza kuwa urasimishaji wa biashara unafanyika kwa kufanya sajili mbalimbali za kibiashara ikiwa ni pamoja na Majina ya Biashara, Kampuni. Alama za Biashara na Huduma,  utoaji wa Hataza, leseni za biashara na  viwanda pamoja na usajili wa viwanda vidogo.

"Urasimishwaji huu unafanyika kwa njia ya mtandao ambapo kwa sasa mfanya biashara hahitaji kusafiri umbali mrefu kupata huduma, maboresho haya tuyatumie kama fursa kwa kuwa sasa sajili zote na utoaji Leseni unafanyika ndani ya muda mfupi sana," amefafanua Bw. Nyaisa.

Kongamano hilo lililoratibiwa na taasisi ya Youth Dreams Foundations limewakutanisha Wajasiriamali Wanawake wa Jiji la Dar es Salaam,  ambao wamenufaika na mada mbalimbali zilizotolewa kuhusiana na ujasiriamali.

Chanzo: Kitengo cha Habari na Mawasiliano BRELA

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.