• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wapiga kura 795,000 Kugawanywa, Jimbo la Dodoma Mjini

Imewekwa tarehe: March 24th, 2025

Na. Faraja Mbise, DODOMA

Halmashauri ya Jiji la Dodoma yawasilisha mapendekezo ya kugawanya Jimbo la Uchaguzi la Dodoma Mjini lenye jumla ya wapiga kura 795,000 na kuwa majimbo mawili, Jimbo la Mtumba lenye jumla ya wapiga kura 412,000 na Jimbo la Dodoma Mjini lenye jumla ya wapiga kura 383,000 kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.

Hayo yalisemwa na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo, Albert Kasoga alipokuwa akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, ya mapendekezo ya mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini, mbele ya Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Jiji la Dodoma. 

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo, alisema kuwa mgawanyo huo umezingatia hali ya kiuchumi ya jimbo husika hasa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani sambamba na kuzingatia ukubwa wa eneo husika.

“Mgawanyo umezingatia hali ya kiuchumi ya jimbo hasa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya jimbo husika. Lengo ni kuona kuwa maeneo yaliyo juu kiuchumi hayamezi kiuwakilishi maeneo yaliyo chini kiuchumi. Aidha, mgawanyo umezingatia ukubwa wa eneo ambapo, Jimbo la Dodoma Mjini lilikuwa na jumla ya Kilomita za mraba 2,478.5. Hivyo, mgawanyo katika majimbo mawili umezingatia eneo hilo ambapo Jimbo la Mtumba lina ukubwa wa kilomita za mraba 1,187.9 na Jimbo la Dodoma Mjini lina ukubwa wa kilomita za mraba 1,290.6” alisema Kasoga.

Kuhusu mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu na huduma za kijamii zilizopo alisema mgawanyo umezingatia hilo kwa weledi mkubwa na ili kuhakikisha wananchi wanasogezewa huduma kwa urahisi.

“Mgawanyo huu umezingatia mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu na huduma za kijamii zilizopo ndani ya kila jimbo, ambapo Jimbo la Mtumba lina jumla ya kata 20 na mitaa 99 na Jimbo la Dodoma Mjini lina jumla ya Kata 21 na mitaa 123, huduma za shule za msingi mgawanyo wake ni shule 59 kwa Jimbo la Mtumba na shule 49 kwa Jimbo La Dodoma Mjini. Shule za sekondari ni 25 kwa Jimbo la Mtumba na Shule 21 Jimbo la Dodoma Mjini. Vituo vya Afya na Zahanati kwa Jimbo la Mtumba ni Zahanati 20 na Vituo vya Afya vinne na Jimbo la Dodoma Mjini lina Zahanati 21 na Vituo vya Afya vitano” alisema Kasoga.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikira, alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, kwa kazi kubwa anayoifanya katika Jimbo lake na kumtakia heri kwa Mwenyezi Mungu ili azidi kuwatumikia wanachi kwa moyo wote.


“Tunakupongeza kwa kazi kubwa unazozifanya kwenye jimbo letu, umefanya kazi kubwa sana mheshimiwa Anthony Mavunde, tunakuombea kwa Mungu akubariki na uweze kuwatumikia watanzania wenzetu” alishukuru Fundikira.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.