Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Girl Guide Association imezindua mpango wa kuhamasisha Lishe kwa vijana wa kike wenye umri wa kuanzia miaka Kumi mpaka 25 Jijini Dodoma, baada ya tafiti kuonesha kuwa vijana wa umri huo wamekua katika hatari ya kutokua na Lishe bora pamoja na upungufu wa damu.
Akizungumza mbele ya kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dodoma, kiongozi wa Utetezi Lishe wa taasisi hiyo Yusta Kobelo amesema kazi yao kubwa ni kutembelea katika shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo ili kutoa elimu ya jinsi gani vijana hao wanaweza kuboresha Afya katika mazingira yao ikiwa ni pamoja na aina ya vyakula, mboga pamoja na matunda.
Kobelo alisema kuwa ndani ya mpango huo wana kampeni inayoitwa Sahani ya Upinde wa Mvua (Rainbow Plate) ambayo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwenye kila sahani anayoishika mtoto wa kike kwa ajili ya chakula iwe na Protini, Vitamini pamoja na Wanga hata kwa uchache ili kutengeneza jamii yenye afya iliyoimarika.
“Imeonekana Wasichana wa sasa hivi wanapenda kuwa na mwili mdogo, wanapenda 'diet' lakini hawajui nini wale nini waache, utakuta msichana anatumia chips kidogo au keki na soda alafu usiku hali kabisa, tunajaribu kuwashawishi kwamba kula ugali na dagaa kwa kiasi kidogo unaweza 'uka-maintain' afya yako, kwa sababu katika vyakula kama hivi kuna virutubisho ambayo vikizidi vinaleta uzito uliozidi na vikipungua vinaleta utapiamlo, kwa hiyo tunatamani wasichana wajifunze mengi kuhusiana na lishe bora” aliongeza Kobelo.
Akizungumzia changamoto walizonazo alisema kubwa ni tatizo la kutokuwa na ofisi Jijini hapa hivyo alimuomba Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuwasaidia kutatuza changamoto hiyo ambapo ikitatuliwa itawasaidia wao kupata nafasi ya kuzungumza na wasichana katika hali ya usiri kwani wapo wenye matatizo ambayo hawawezi kuyazungumza hadharani lakini wakiwa na ofisi itawasaidia kuwa karibu nao zaidi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.