• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wataalam wa Jiji la Dodoma kuweka kambi Ndachi

Imewekwa tarehe: May 14th, 2023

WATAALAMU wa Jiji wakiongozwa na mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru wamejipanga kuweka kambi Kata ya Mnadani mtaa wa Ndachi ili kutatua migogoro ya ardhi iliyoibuka katika hatua ya mwisho ya ugawaji wa viwanja kwenye eneo la hilo.

Mafuru  aliyasema hayo alipohudhuria mkutano wa kusikiliza malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Ndachi, Kata ya Mnadani uliofanyika katika shule ya msingi Ndachi jijini hapa.

Mafuru alisema kuwa Jiji la Dodoma limekuwa likipokea  malalamiko mengi sana ya ardhi kutoka kwa wananchi wa Ndachi ambayo  yamekuwa yakipelekwa kwa namna tofautitofauti. “Ndugu zangu wa Ndachi tumekuwa tukipokea malalamiko mengi sana, kuna wanaokuja moja kwa moja ofisini, wanaoukuja kwa barua, wanaokwenda mkoani na Wizara ya Ardhi Mtumba.

Tutaweka kambi siku 21, naamini tukikaa Ndachi kwa muda wa siku 21 hakuna kitu tutakiacha. Ndachi nitaweka wataalam wanne ambao sio kutoka ardhi, wawili watakuwa wa sheria wengine watakuwa kutoka Maendeleo ya Jamii na Mazingira. Naleta watu ambao sio maafisa wa ardhi ili wawe ‘neutral’  wasifanye kazi kwa kushawishiwa na wataalam wa  ardhi, tutafanya kazi kwa siku tano halafu tutakutana kwaajili ya mkutano wa tathmini” alisema Mafuru.

Aidha, alielezea namna zoezi hilo la kutatua migogoro ya ardhi Mtaa wa Ndachi linavyoenda kutekelezwa. “Tunamabalozi 86 na wanaaminika sana. Mabalozi ndio wanajua watu wao wote, wanajua nani kahudumiwa na nani  hajahudumiwa,  tunaenda kushirikiana nao watusaidie kumalizia hatua ya mwisho ya ugawaji. Tutaanza na Mtaa wa Ndachi, tutagawa timu mbili,  timu moja eneo la Matuli na nyingine Ndachi. Tutakaa kwa siku tano, wenye changamoto kuanzia leo mkajiorodheshe kwa mabalozi wenu  ndani  ya siku hizo njoo na lalamiko lako lolote iwe mipaka, ‘invoice’, mapunjo ya asilimia za ugawanaji wa viwanja  njoo na kitu chochote usichoridhika nacho. Tutaenda kuongeza kasi ya utoaji wa hati ndani ya hizo siku tano tukimaliza tutahamia Mtaa wa Mbwanga na Karume.

Akitoa malalamiko yake kwenye mkutano huo mkazi wa Ndachi, Abilai Sharifu alisema “Mkurugenzi ondoa wote unda kamati mpya kama kamati itaendelea kubaki na kuwa na watu walewale  hatuwezi kupata haki sababu kamati hiyo ndio wapigaji wakuu. Kwanza kwenye kamati ya ardhi kuna wengine wameingia wanasiku 20 tu, sisi ndio wanandachi hatuwezi kutatuliwa matatizo yetu na mtu asiye mkazi wa Ndachi matatizo ya wananchi wa ndachi yatatatuliwa na mwanandachi. Ni ombi langu Mkurugenzi uvunje kamati yote sababu hawajachaguliwa na wananchi wa Ndachi.

Wakati huohuo Mkazi wa Matuli, Mohamed Mamba alisema kuwa migogoro ya ardhi kwenye Mtaa wa Ndachi haiwezi kuisha kama wananchi hawatashirikishwa katika kuunda kamati itakayosimamia matatizo yao.   “Ukitaka hii hali iishe kila sehemu ya mji wa Dodoma weka kamati itakayochaguliwa na wananchi wenyewe wanaowaamini sio wanachaguliwa na viongozi. Kamati ndizo zitashughulikia migogoro ya ardhi, unda kamati kila mtaa watakayoikubali wananchi kwa idadi itakayotakiwa uitambue na mtaa uitambue kamati hiyo ndio ipewe jukumu lakusimamia zoezi la ugawaji wa viwanja“ alisema Mamba.

Akielezea historia  ya mradi wa upimaji Ardhi Ndachi Afisa Upimaji  Ardhi Jiji la Dodoma,  Luis Kiwale alisema kuwa mradi wa upimaji wa ardhi Ndachi ulianza rasmi 2018 ukihusisha zoezi la uhakiki, upangaji , upimaji na sasa mradi upo kwenye hatua ya mwisho ya  ugawaji. Zoezi la ugawaji wa viwanja kwenye Mtaa wa Ndachi linahusisha watu wa aina mbili ambao wote ni wanufaika wa mradi, kuna wamiliki wa mashamba na wananchi wazawa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.