Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kukabiliana na ugonjwa wa Corona ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu nchini.
Kauli hiyo imetoliwa leo na Mheshimiwa Waziri Mkuu baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa king, fedhas na ddawa kutoka taasisi, kamapuni na umoja wa mama ntilie nchini.
Mheshimiwa Kaasim Majliwa amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuzingatia kuchukua tahadhari kama vile kunawa mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na kuepuka misongamano ili kudhibiti janga hili kubwa lililoyakumba pia mataifa makubwa. "Wakati tunaendelea kukabliana na janga hili la Corona pia tunapaswa kujua kwamba ugonjwa huu utaleta athari za kiuchumi" amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu amewashukuru Watanzania waliojitokeza kuchangia fedha, dawa na vifaa kinga kwa kuwa msaada huo utasaidia watu wote waliokumbwa na Covid-19 pamoja na kusaidia Watanzania kujikinga ili kuzuia kusambaa kwa home kali ya mapafu. "Hivi vitu vyote tulivyopokea leo ni gharama kubwa, tumeona Watanzania wenye moyo wamekuja hapa kuungana na Serikali kukabiliana na ugonjwa huu, hivyo hatuwezi kuacha hivi bila kutoa shukrani kwa wenzetu waliotoa msaada huu". amesema Mhe. Majaliwa.
Amesema Watanzania wanaopenda kuchangia jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu, wachangie fedha Benki Kuu kupitia akaunti ya National Relief Fund Electronic, namba 9921159801 na kwamba wanaweza kuchangia kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Waziri wa Afya, Maendeleoa ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Baadhi ya Kampuni zilizochangia Serikali katika kukabiliana na Corona ni Benik ya NMB milioni 100, CRDB Milion 150, Benki ya UBA milioni 230, umoja wa mama ntilie milioni 2, Ashton Media milioni 104 na Kampuni mbalimbali zimechangia fedha na vifa kinga kwa lengo la kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Picha za baadhi ya matukio:
Chanzo: wizara_afyatz (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.