WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka watanzania waunge mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza kwa bidii filamu ya Royal Tour pamoja na vivutio mbalimbali vilivyoko nchini.
Ametoa wito huo leo usiku (Jumapili Mei 15, 2922) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma waliofika kushuhudia uzinduzi wa filamu hiyo, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
“Baada ya hapa, wana Dodoma twende tukaisemee filamu hii kwa kutumia simu zetu na mitandao ya kijamii,” amesema Waziri Mkuu ambaye alikuwa akimuwakilisha Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Amesema kuzinduliwa kwa filamu ya Royal Tour kumefungua zaidi milango ya utalii kwani baada tu ya uzinduzi Tanzania ilipokea watalii 796 kutoka Israel ambao walikuja kwa ndege tatu zilizofuatana.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka Wakuu wengine wa Mikoa watenge siku moja na kuwashirikisha wananchi wao washuhudie kazi kubwa ambayo imefanywa na Mheshimiwa Rais.
“Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Mtaka yeye kaanza. Ni vema wakuu wenginge wa Mikoa watafute siku moja ya kuwaonesha watu wao, wanaweza kuchagua hata kwenye ngazi ya Halmashauri ili juhudi za Mheshimiwa Rais wetu.” Amesema kwa ufafanuzi.
Vilevile, ameeleza kuwa kitendo cha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuruka kwa ndege na kuonesha kwa karibu kilele cha Mlima Kilimanjaro, kimekata mzizi wa fitina juu ya mahali halisi ulipo mlima huo. “Mheshimiwa Rais amekata mzizi wa fitina na kuithibitishia dunia kuwa Mlima Kilimanjaro uko Tanzania.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.