WATANZANIA wanahitaji elimu zaidi ili waweze kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa kisukari ambao umekua ukiongezeka nchini.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Petro Sabato kwenye madhimisho ya siku ya Kisukari Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza.
"Elimu inahitajika zaidi ili kuwakinga wananchi na Magonjwa Yasiyoambukiza hasa Kisukari kwa kuwa ugonjwa wa Kisukari umekua ukigharimu maisha ya watu ikiwa ni pamoja na kukatwa baadhi ya viungo ." Amesema Bw. Sabato
Aidha, Bwa. Sabato ametoa rai kwa wananchi kufanya mazoezi sambamba na kupima Afya angalau mara moja kwa mwaka ili ukigundulika mapema inakuwa rahisi kupata matibabu.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza Bi. Valeria Milinga amesema vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza yanachangia kwa asilimia 33 huku ugonjwa wa kisukari ukiwa ni 9.10%
"Katika kuongeza uhamasishaji na uelewa kwa wananchi juu ya magonjwa yasiyoambukiza hasa ugonjwa wa kisukari tumeweza kufanya maonyesho ya wiki ya magonjwa
yasiyoambukiza yaliyoanza tarehe 5-12, Novemba 2022 ambayo yanafanyika kila mwaka." Amesema Bi. Milinga
Aidha, Bi. Milinga ametaja mafanikio ya maonyesho hayo kwa mkoa wa Mwanza hadi kufikia siku ya kilele tarehe 12, Novemba, 2022 wananchi takriban 3000 wamejitokeza kupima
ugonjwa wa kisukari na 34 kati yao wamegundulika kuwa na ugonjwa huo.
Hata hivyo, amebainisha mafanikio waliyoyapata katika utoaji wa huduma za kisukari ikiwemo upatikanaji wa Dawa, utoaji wa mafunzo kwa watoa huduma za Afya katika Vituo 300 kwenye
Mikoa 9.
Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Kisukari Tanzania Prof. Andrew Swai amesema miaka ya 1991 kulikuwa na 1% tu ya ugonjwa wa kisukari nchini lakini kwa sasa imeongezeka hadi kufikia 9%.
"Kutokana na ongezeko la ugonjwa wa kisukari nchini imekua tatizo ambapo inagharimu 20% ya bajeti ya Serikali ili kuwahudumia wagonjwa hao." Amesema Prof. Swai
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.