Na. Dennis Gondwe, DODOMA
USHIRIKIANO baina ya watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni njia pekee ya kuleta ufanisi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyojitika kuwaletea maendeleo wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba alipotoa salamu za CCM katika Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mamba alisema kuwa ushirikiano baina ya watumishi na madiwani ni muhimu sana katika kutekeleza kazi za halmashauri. “Watumishi twende pamoja, tunazungumzia suala moja na watumishi kwa sababu ni watekelezaji wa Ilani ya CCM. Niwaombe watumishi wapeni ushirikiano wa kutosha waheshimiwa madiwani. Mkurugenzi shirikiana na madiwani na washauri vizuri. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma sina shaka na ofisi yako, umekuwa ukitenda vizuri na wakati mwingine tukikwambia waziwazi hapa bila wewe tungeshindwa. Nataka tujenge nyumba kwa upendo na kushauriana” alisema Mamba.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.