Na Shaban Ally, DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri awashauri watumishi wa umma kutendea haki ongezeko la asilimia 23.3 ya mishahara yao iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya kazi kwa uadilifu na ubunifu kwa kuzingatia haki na maslahi mapana ya nchi.
Ushauri huo aliutoa leo katika hafla fupi ya kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha maslahi ya watumishi katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF jijini hapa.
“Kutokana na juhudi na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, sisi kama watumishi wa umma tusishangilie ongezeko la mishahara bali tunapaswa kutendea haki mishahara iliyoongezwa na Mheshimiwa Rais" alisema Shekimweri.
Mkuu wa wilaya huyo alitoa rai kwa watumishi wa umma kuboresha maisha yao katika kipindi hiki cha ongezeko la mishahara. Alisema kuwa watumishi wengi wa umma wamekua wakiishi maisha ya taabu kutokana na kutokuwepo na matumizi mazuri ya mishahara yao.
Aidha, alimpongeza Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa tuzo ya uendelezaji wa miundombinu na Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi 100 bora wenye ushawishi duniani walioorodheshwa kwenye jarida la kimataifa la Forbes.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.