• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Watumishi timizeni matarajio ya Rais Samia - Majaliwa

Imewekwa tarehe: October 19th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma watimize wajibu wao kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia wafanye pindi anapowateua ama kuwapa ajira.

"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona watumishi wa umma mkiwatumikia Watanzania. Nenda kwa wananchi mkawasikilize. Huwezi kuwahudumia bila kuwasikiliza na huwezi kujua changamoto zao bila kuwasikiliza," amesema.

Ametoa wito huo leo mchana (Jumatano, Oktoba 19, 2022) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa, wilaya na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwenye ukumbi wao mara baada ya kuzindua jengo la Halmashauri hiyo.

Amewataka viongozi na watumishi hao wafanye kazi kwa kulenga matokeo. "Nataka tufanye kazi kwa matokeo, tufuate maelekezo na tuzingatie nidhamu. Tuna fedha za ndani na za Serikali Kuu. Tuzisimamie vizuri na naomba msijiingize kwenye matumizi mabaya ya fedha hizo," aliwaonya.

Waziri Mkuu aliwapa mfano wa Mkuu wa shule ya sekondari Irugwa ambaye alipokea sh. milioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa sita, lakini alizisimamia vizuri akamaliza madarasa, akajenga matundu matano ya vyoo, kuweka mfumo wa maji ya mvua na chenji iliyobakia akapiga lipu mabweni ya wasichana na kujenga mabafu licha ya kuwa shule iko kisiwani na kisiwa kiko mbali kutoka Nansio (makao makuu ya wilaya) na pia kiko mbali kutoka Mwanza ambako mahitaji yote yanafuatwa.

"Nanyi pia fanyeni hayo hapa Madaba, mtumishi wa umma jitahidi ufanye jambo ambalo wengine limewashinda. Mheshimiwa Rais Samia anatamani kuwa na watumishi wengi wa aina hiyo."

Kuhusu hoja za CAG, Waziri Mkuu amesema Halmashauri hiyo ya Wilaya ilikuwa na hoja 46 ambapo hoja 28 zimefungwa na hoja 18 bado hazijafungwa. "Malizieni hoja hizi 18 zilizobakia," amesisitiza.

Kuhusu ujenzi wa hospitali ya Halmashauri hiyo, Waziri Mkuu amewataka wakamilishe ujenzi kwa viwango alivyoviona na akampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Sajidu Mohammed kwa usimamizi mzuri.

Mapema, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kuweka jiwe la msingi. Ujenzi wake umeshatumia sh. bilioni 2.084.

Akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa hospitali hiyo na kwamba anataraji hatua ya ukamilishaji itazingatia viwango bora.

Naye, Mbunge wa Madaba, Bw. Joseph Mhagama alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia wana-Madaba sh. bilioni 14.2 ambazo zimetumika kujenga miradi ya maji, barabara za vijijini, miundombinu ya afya na elimu.

Alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali iwajengee kituo kikubwa cha mabasi na soko kubwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.