WAWEKEZAJI wamekaribishwa kutembelea na kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa jengo la kitegauchumi “Government City Complex” mradi unaojengwa kwenye Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Mchumi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fred Robert (pichani) alipokuwa akiwasilisha mada juu ya fursa za uwekezaji katika Jiji la Dodoma kwenye mkutano wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) uliofanyika katika hoteli ya Dar es Salaam Serena.
Akiongelea fursa za uwekezaji katika kitegauchumi hicho, Robert alizitaja kuwa ni ‘diplomatic apartments’, migahawa, maduka makubwa, kumbi za mikutano, maegesho ya magari, maeneo ya ofisi na maeneo ya huduma za kibenki.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF), Zachy Mbenna aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwafikiria wawekezaji wa ndani na kuwatembelea katika mkutano wao. Aidha, aliahidi kuwa taasisi yake itakuwa balozi wema wa uwekezaji kwa Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.