• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Dkt. Gwajima aagiza kuundwa kamati kuonesha mchango cha NGOs nchini

Imewekwa tarehe: September 10th, 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu kuunda Kamati maalum itakayofanya tathimini ya mtawanyiko na mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa.

Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya maazimio ya kikao cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika Januari, 2021 na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Mashirika hayo ili kuleta maendeleo endelevu ya Taifa kwa ujumla.

Agizo hili limekuja kutokana na maazimio na mapendekezo ya Mashirika hayo kwa Serikali ya kufanya tathmini ya mchango wa Mashirika hayo katika kuleta maendeleo kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwa na taarifa sahihi za Mashirika yapi yamefanya nini katika eneo gani

Waziri Gwajima ameongeza kuwa Wizara itahakikisha kunakuwa na usimamizi mzuri wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili yaweze kusaidiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imejinasibu katika kushirikiana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuwaletea maendeleo wananchi katika Maeneo mbalimbali" alisema Dkt. Gwajima.

Aidha ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia uwazi na uwajibikaji kwa kuhakikisha fedha wanazozipokea kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zitumike kwa kadiri ilivyotarajiwa ili kuleta matokeo chanja katika jamii.

Amesema uwepo wa uwazi na uwajibikaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini utasaidia Serikali kupata taarifa ya miradi inayotekelezwa na Mashirika hayo na kwa namna gani imesaidia wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Akitoa taarifa ya maazimio ya kikao cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Naibu Mkurugenzi wa Mpango wa Uwajibikaji Tanzania (Accountability in Tanzania Program) Rehema Tukai amesema kikao kilichofanyika kilitoka na mazimio matano ambayo yamelenga katika kuhakikisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini yanashirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Revocatus Soro amemhakikishia Waziri kuendelezwa ushirikiano miongoni mwa Mashirika na kati ya Mashirika na Serikali ili kuhakikisha Sekta ya NGOs nchini inatoa mchango kwa maendeleo ya jamii.

Wakati huo huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amepokea mwaliko wa Mkutano wa Mwaka wa NGOs utakaofanyika tarehe 29-30, Septemba, 2021. Jijini Dodoma.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.