• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jafo aelekeza NHC ivune maji Dodoma

Imewekwa tarehe: September 1st, 2021

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo ameelekeza mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Iyumbu jijini Dodoma kujenga mfumo wa uvunaji maji ili yasitiririke na kusababisha athari za kimazingira katika Mji wa Dodoma.

Jafo ametoa maelekezo hayo leo Septemba mosi, 2021 alipofanya ziara ya kikazi katika mradi huo wa ujenzi kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Hata hivyo, alionesha kutoridhishwa na kukosekana kwa mifumo ya uvunaji maji na kuelekeza uongozi unaosimamia mradi kushirikiana na mamlaka zinazohusika na masuala ya usimamizi wa maji kuhakikisha wanajenga mifumo hiyo. 

“Hapa sioni mifumo ya uvunaji wa maji ya mvua, haya mabati yatamwaga maji mengi na kusababisha mafuriko. Leo hii kule Nkuhungu nyumba zimezama kwa mafuriko, soko la Ndugai na stendi ya Dodoma na maeneo mengine yatajaa maji sasa tukiwa na system ya uvunaji maji tutapunguza mafuriko na pili tutafanya management (usimamizi) ya maji,” alisema.

Pamoja na hayo pia alizitaka mamlaka zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi kuhakisisha vibali hivyo vinawataka waombaji kujenga mifumo ya uvunaji maji katika miradi hiyo ili kuzuia maji yasitiririke ovyo na kusababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo ya miji.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo katika ziara hiyo iliyolenga kukagua uzingatiaji wa uhifadhi wa mazingira alitoa maelekezo kwa wakandasi kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo ya miradi wanayojenga.

Alisisitiza kuwa kuwa agenda ya mazingira iwe kipaumbele cha kwanza katika miradi mikubwa inayotekelezwa nchini na kwamba wakati wa maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo, eneo hilo lilifyekwa miti hivyo kuna ulazima wa kupanda miti kwa wingi ili kuliweka katika mazingira mazuri.

”Hizi projects (miradi) kubwa wakati mnazitekeleza lazima agenda ya mazingira iwe kipaumbele cha kwanza kwasababu ukiangalia hili eneo hapa msipopanda miti litakuwa ni eneo la ajabu sana, hapa kwanini msipande miti ya matunda mtu atapata embe na wakati huo anakuta mmetunza mazingira,”  alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri alisema  pamoja na mradi huo wa nyumba kuwa ni mzuri lakini una changamoto mbalimbali.

Alisema miongoni mwa changamoto hizo ni kutokufuatwa kwa masharti ya mkataba wa ujenzi ambao ni kumtaka mkandarasi pamoja na mshauri kufanya kazi bega kwa bega na wadau kama Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ili kupata ushauri usimamizi wa maji.

Shekimweri alisema kuwa ipo haja sasa wakati wa utoaji wa vibali vya ujenzi kuwataka waombaji kupanda mitano ikiwemo ya matunda na ya kivuli ili kuhifadhi mazingira.

Pia aliiomba Serikali kupitia kwa Waziri kuelekeza wakandarsi kusimamiwa kipengele cha kushirikisha wadau muhimu wakiwemo Jiji wakati wa utekelezaji wa miradi ili kuepuka madhara ya kimazingira yanayoweza kutokea.

Naye Mkurugenzi wa Ujenzi wa NHC, Bw. Haikameni Mlekio alisema wameyapokea maelekezo ya Waziri Jafo na kuahidi Uongozi wa Shirika hilo utayafanyia kazi. 

Katika ziara hiyo Waziri Jafo aliambatana na Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Meneja kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)-Dodoma, Patricia Manongi na Afisa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Deogratius Paul na Afisa kutoka NEMC, Emmanuel Mwasilu.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.