MIFUMO ya ukusanyaji wa mapato katika kituo cha Makole imesaidia kuinua kiwango cha ukusanyaji katikakituo hicho kutoka shilingi milioni 9 hadi milioni 25 kwa mwezi.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho George Matiko alipokuwa akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo alipotembelea kituo hicho leo Jumatatu Agosti 3, 2020.
Ziara hiyo ya Waziri Jafo ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Afya ya TAMISEMI iliyoanza kwa mazoezi ya viungo yaliyoongozwa na Waziri Jafo katika uwanja wa shule ya Sekondari Dodoma kuanzia saa 12:30 asubuhi.
Kufuatia mapinduzi hayo makubwa ya ukusanyaji wa mapato katika kituo hicho, Matiko aliishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kukiboresha kituo hicho kwa kuongeza miundombinu pamoja na kuweka mifumo ya mapato.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.