• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Jafo atoa siku 7 ujenzi Hospitali ya Uhuru uanze

Imewekwa tarehe: June 19th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo ametembelea eneo  la Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru na kuagiza uongozi wa Serikali ya Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuhakikisha ujenzi huo unaanza ndani ya siku saba.

Ikumbukwe kuwa Jumanne ya Novemba 20, 2018 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitoa tangazo la maagizo ya Mh. Rais John Magufuli yaliyooelekeza kiasi cha Sh milioni 995.182 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe za Uhuru Desemba 9 mwaka jana, zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo wilayani Chamwino ambayo itakuwa ya kisasa na teknolojia za hali ya juu zitatumika kutoa matibabu. Hata hivyo Serikali imetenga fedha nyingi zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Hospitali hii.

Katika ziara hiyo ambayo waziri aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge, waziri Jafo alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Chamwino na kuwataka watumishi kushirikiana na kudumisha upendo miongoni mwao.

Aidha Mh. Waziri amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Bwana Masasi  na watumishi wote kwa kutii agizo la kuhamia kwenye ofisi mpya za Halmashauri ya Chamwino zilizopo eneo la Buigiri.

“Nimefurahishwa sana kuona sasa watumishi mmehamia katika ofisi zenu. Niagize tena SUMA-JKT kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanakamilisha kazi zao za msingi katika jengo hili”. Alisema Mh. Jafo

Vilevile Mh. Jafo ameitaka Halmashauri kuongeza kasi ya upimaji wa viwanja ili kuhakikisha Chamwino ambapo ni makazi ya Rais panapangika vizuri na kusema kuwa upimaji wa viwanja utaongeza thamani ya ardhi na itaiongezea mapato Halmashauri. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. Masasi amemueleza waziri kuwa ameshapokea kiasi cha shilingi mil. 500 kwa ajili ya kutekeleza zoezi la upimaji wa viwanja.

Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Samwel Kaweya amemshukuru waziri na kuahidi kuwa madiwani watashirikiana na wataalam kuhakikisha maagizo yote yanatekelezwa.

Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, inapakana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma (Chamwino iko upande wa mashariki wa Jiji la Dodoma).


Chanzo: Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino (www.chamwinodc.go.tz)


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.